Thursday, 30 April 2020Ufugaji kwa sasa ni moja ya ufugaji mzuri sana hapa nchini na nje ya nchi,licha ufugaji huu kuendelea vizuri lakini hakuna changamoto zinakosekana katika shughuli husika unayoifanya,huenda ufugaji samaki indio ikiwa inachangamoto ndogo kabisa kuliko ufugaji mwingine kama vile kuku,bata,mbuzi ,ngombe na mifugo mingine.Elimu ya ufugaji wa samaki kwa miaka ya karibuni imekuwa ikiwafikia wengi sana na hii kutokana na ufikiaji wa taarifa kwa haraka kupitia vyombo mbalimbali za habari,kama vile redio,tv,magazeti na majarida,hivyo kuendelea kufanya miradi ya ufugaji wa samaki kuendelea kuwa na tija zaidi kutokana na uelewa mpana zaidi kuhusu ufugaji wa samaki.Ukweli halisi ni kwamba wafugaji wengi au wengine wanaotarajia kuingia kwenye ufugaji wa samaki wanafahau vitu mbali mbali kuhusu ufugaji samaki,baadhi ya mambo hayo muhimu ikiwemo ufahamu sahihi juu upandikazaji wa idadi sahihi kupandikiza samaki ndani ya bwawa tofauti na awali wafugaji wengi walipandikiza samaki wengi sana kwenye bwawa dogo kinyume kabisa na taratibu na kanuni za ufugaji na endapo mfugaji ataweka samaki wengi katika bwawa dogo basi hapo utakuta mfugaji huyo anabadilisha maji mara kwa mara au anatumia mifumo ya kuongeza hewa ndani bwawa,ulishaji wa chakula na utengenezaji wake,ubadirishaji wa maji na ujenzi bora wa mabwawa ambayo yanakuwa na mifumo mizuri ya utoaji wa maji,hizo ni mojawapo tu za mada au masomo mbalimbali ambayo yameshatolewa na jarida hili,kupitia mada hizo baadhi ya wafugaji samaki wameweza kuondokana au kupunguza idadi ya changamoto hizo kwa ufasaha zaidi.
Licha na mafaniko mbalimbali baadhi ya changomoto zinajitokeza kwa baadhi ya wafugaji na moja ya changamoto kuu na uwepo wa vifo vyasamaki,wapo wafugaji ambao hukuta samaki wao hufa  moja moja kila siku,mwingine wanakufa watatu ,watano au kumi kwa siku na wingine pia kutokea samaki wote wamekufa kwa siku moja,wafugaji wengine samaki hupunguza kasi na matarajio kwa sababu ya vifo samaki vinapotokea kwenye bwawa lake,pasi kujua baadhi ya vifo vinatokana nay eye ,mwenyewe kutozingia maelezo sahihi ya ufugaji nikiwemo usafi wa  maji kwenye bwawa husika na sababu kadhaa ambazo tutazileza hapa kwanini vifo vya samaki vinatokea kwenye bwawa lako.
INAENDELEA

Friday, 21 February 2020

NJIA HIZI NI MUHIMU SANA KATIKA UHIFADHI NA UCHAKATAJI WA SAMAKI WAKO.


Kukausha kwa jua: Njia ya kuchakata samaki kwa kutumia nishati ya jua ili kuondoa maji na kuondoa vimelea na kuvifanya visilete uharibifu wa samaki. Gharama ya nishati ni rahisi Kupunguza gharama za ujazo ,Aina ya wateja ulionao na soko Kurahisisha ubebaji na ufungashaji Gharama ya vifaa vinavyohitajika si vya gharama kubwa
CHANGAMOTO ZA KUKAUSHA KWA JUA: Haitumiki wakati wa kipindi cha mvua au mawingu, Inahitaji eneo kubwa la uchakataji ,Unahitaji muda mrefu kukamilisha uchakataji ,Unahitaji idadi kubwa ya watendaji ,Kuongeza gharama ya kuandaa vichanja
 KUKAUSHA KWA CHUMVI : Njia ya kuchakata samaki kwa kutumia madini ya chumvi ili kuondoa maji na kuondoa vimelea na kuvifanya visilete uharibifu wa samaki. Eneo dogo uhitajika kwa ajili ya uchakataji, Gharama ya kuthibiti muingiliano ndani ya eneo la uchakataji ni ndogo ,Inaongeza radha na madini katika aina ya zao ,Haitegemei sana hali ya hewa ,Inapunguza kasi ya ukuaji wa vimelea vinavyopelekea kuharika kwa samaki.

KUKAUSHA KWA MOSHI : Njia ya kuchakata samaki kwa kutumia moshi ili kuondoa maji na kuondoa vimelea na kuvifanya visilete uharibifu wa samaki. Inahitaji eneo dogo la kufanya uchakataji, Haitegemei hali ya hewa kuwezesha uchakataji ,Inaongeza muonekano na rangi ya kuvutia katika bidhaa, Inaongeza muda wa kuhifadhi na utunzaji wa bidhaa
KUKAANGA: Njia ya kuchakata samaki kwa kutumia mafuta ya kula kwa kukaangia ili kuondoa maji na kuondoa vimelea na kuvifanya visilete uharibifu wa samaki. Inaongeza radha ya aina ya bidhaa ,Inahitaji eneo dogo la kufanya uchakataji ,Haitegemei hali ya hewa kuwezesha uchakataji ,Inaongeza muonekano na rangi ya kuvutia katika bidhaa, Inaongeza muda wa kuhifadhi na utunzaji wa bidhaa Gharama ya upatikanaji wa nishati ni ndogo, Inahitaji muda mfupi kukamilisha uchakataji.
KUGANDISHA NA KUPOZA KWA KUTUMIA BARAFU :njia ni moja ya njia kuu ya uchakataji katika kuhifadhi samaki wakati unajiaanda kupeleka sokoni,faida kubwa ya kutumi njia kuwa, Inahitaji muda mfupi kukamilisha uchakataji Inalinda uasili wa bidhaa Unaweza kusafirishwa umbali mrefu.
Hizi ndio njia kuu ambazo zinapelekea kuboresha samaki wako pindi au unapojiiandaa kupeleka sokoni ukizingatia haya na kwa kushirikiana na mtaalam kwa ukaribu zaidi unaweza kufaniwa zaidi na kuepukana na changamoto ambazo ulikuwa unakutana nazo wakati unapokaribia kuvana samaki wako.

Tuesday, 18 February 2020

UNAWEZAJE KUFANYA SAMAKI WAKO WASIHARIBIKE HARAKA BAADA YA KUVUNA?.
Ufugaji samaki kwa sasa unashika kasi sana,katika kuhakikisha kuwa mfugaji anaweza kufanikiwa katika hatua zote za ufugaji wake mpaka hatua ya kupeleka bidhaa yake sokoni katika ubora ili isipunguze thamani ya samaki wake.Samaki kama viumbe vingine visipohifadhiwa vizuri na katika utaratibu maalum wa kitaalam wanaharibika na kuoza hivyo kama umefuga samaki kwa kipindi cha miezi sita mpaka saba kisha unakuja kuvuna samaki wako unashindwa kufuata kanuni bora za uhifadhi wa samaki wako inakuwa changamoto mpya ambayo pengine hukuweza kuiwaza na kuifikilia kama inaweza kutokea.Ili kuepukana na majuto hayo mkulima mbunifu itakuelimisha njia bora imbayo itakusaidia kuhakikisha samaki wako unapowavuna kitu gani muhimu unapaswa kukifanya ili samaki wawe katika ubora  unaohitajika sokoni.
Kitu muhimu na chakuzingatia cha awali ni kuhakikisha wakati unafuga soko lako umelenga kuuza samaki kwa wateja wa aina gani,mfano unapofuga samaki unaweza kusema mimi nataka niuze mwenyewe kwa reja reja hapo maana yake utakuwa unavua bwawani na kumuuzia mteja samaki ukiwavua moja kwa moja kutoka bwawani,njia ya pili unawauza wote kwa pamoja yaani inawezekana umewaalika watu waje shambani baada ya kufanya matangazo kuwa siku fulani nauza samaki wangu hivyo siku husika wale wanunuzi watafika shambani na kuwauzia samaki hapo hapo,njia ya tatu unataka uuze kwa kuwasafirisha na kupeleka sokoni mwemyewe yaani unavuna unapakia kwenye vyombo na kisha kupeleka sokoni mwenyewe,katika hili la kupeleka sokoni kuna njia mbili njia ya kwanza kuwavuna samaki kupeleka wabichi sokoni na njia ya pili kuwavuna na kupeleka wakiwa umekausha samaki wakiwa wakavu.Katika kipengili hichi chote tunakugusa kuwa soko lako umelilenga vipi,kwa nani na kwa namna gani kulingana na mahitaji husika ya soko,kumbuka ufugaji samaki umetofautiana sana kulingana na ukubwa wa bwawa mathalani kuna wengine wanafuga samaki 100 kuna wengine wanafuga samaki 10,000 na kuendelea.Kuna wengine wanafuga sato na wengine wanafuga kambale hivyo katika hatua zote hizo kuna umuhimu mkubwa sana wakutambua kama una idadi ndogo au kubwa utawahikikisha vipi samaki wako wanabaki na ubora mpaka kufika sokoni.
Kwa wafugaji ambao wamefuga na lengo kuu ni kuuza kidogo kidogo hapa tunashauri sana kuhakikisha kuwa wanaepuka unavuaji wa mara kwa mara kuingia ndani ya bwawa,kufanya hivyo unaweza kupelekea kuwapa michubuko samaki wengine wakati unavua kwa kutumia  nyavu,mfano amekujawa mteja wa samaki anahitaji kilo moja umevua,baada ya nusu saa kaja mteja mwingine umevua kitendo hicho cha mara kwa mara unaweza kupelekea vifo kwa samaki wengine na kuanza kuharika pasi kujua hivyo inapelekea kupunguza ubora na kiwango ulichokusudia kuuza samaki wako.Njia bora na pekee ambayo ni salama itahakikisha kuwa samaki watakuwa na ubora ,kama bwawa lako ni kubwa hakikisha unakuwa na neti maalum ya kuwahifadhia kwa kitaalam inaitwa HAPPANET neti inashonwa kwa ukubwa maalum kulingana na nafasi ya bwawa lako mfano bwawa lako lina ukubwa wa mita 10 kwa mita 10 unaweza kushona au kununua nyavua hiyo kwa ukubwa wa mita tano kwa tau unafunga ndani ya bwawa,unavuna samaki wako kiasi mfano kama unasamaki mia tano unavuna samaki mia mbili kisha unawaweka ndani ya hiyo neti hapo itakuwarahisi sana mteja anapokuja kunyanyua hiyo neti na kuchukua samaki anahitaji hivyo wale wakwenyewe bwawa wanakuwa haguswi tena kufanya hivyo mteja anapata kilicho bora na uhifadhi huu ni wa gharama nafuu sana kulinganisha na uhifadhi wa kwenye jokofu au barafu hususani katika idadi hiyo na aina yawateja kwa reja reja,matumizi ya jokofu pia inawezekana ila gharama ya nishati ni kubwa lakini pia endapo nishati hiyo inakosekana uwezekano wa kuharibika ni mkubwa.
Hakikisha unavuna samaki wako unakuwa na vifaa vya kutosha vya kuwahifadhia baada ya kuvua samaki wako ni vema sana ukawa na mabarafu pindi unapovuna kuwahifadhi humo ndani ya mabeseni ili samaki hao wasiharike haraka,toa mautumbo ya samaki wako ili wasiharike utoaji wa mautumbo ya samaki yatasaidia sana kuhakikisha kuwa samaki wanabaki katika ubora mkubwa na kufika soko pasi na shaka yeyote ile,au kama unasamaki wengine hakikisha unakuwa na usafiri maalum wenyekuzalisha barafu VAN CAR ni magari maalumu kwa ajili kusafishia samaki kwa umbali mrefu zaidi.

Tuesday, 4 February 2020

TUJIKUMBUSHE KIDOGO MAANA HALISI YA UFUGAJI SAMAKIHili ni swali la msingi kabisa kufahamu ili ikusaidie kufahamu kitu unachotaka kutekeleza.
Ufugaji wa samaki ni kazi ya kupanda,kukuza na kutunza samaki katika bwawa au uzio (uliotengenezwa kwa vyuma,miti pamoja na nyavu) au eneo lolote ambao uthibiti wake uko chini ya mamlaka ya mfugaji mwenyewe.Mabwawa yanaweza yakawa ya kuchimbwa na watu(japo kuwa mabwawa ya asili pia yanaweza kufugia samaki) wakati yale yanaweza yakawekwa katika eneo lolote lenye maji mengi kama vile ya ziwa,mto au bahari.
Ufugaji wa samaki katika kiasi Fulani si sawa na ukuaji wa samaki katika mito,maziwa na bahari.Tofauti kubwa iliyopo samaki wanaofugwa na wasiofugwa ipo katika huduma,huduma wanazopata samaki wanaofugwa huwekwa kwa idadi maalumu ndani ya bwawa,kupatiwa chakula na kuhudumiwa vizuri.
Ufugaji wa samaki sio kitu kipya kabisa hapa Tanzania,baadhi ya watu wamekuwa wakifuga samaki kabla ya hata kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika.Lakini baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitoa matunzo hafifu kwa samaki hao,hivyo kupelekea mavuno hafifu katika ufugaji huo.kwa miaka ya hivi karibuni serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikitilia mkazo katika utoaji wa elimu (ugani) ili kuboresha mafanikio yake yaweze kupatikana kama nchini nyingine zinazotekeleza miradi hii.Kupitia muongozo wa mafunzo haya kila mtu atafahamu faida ya ufugaji na namna ya kuwafuga samaki wake ili waweze kukua vizuri na kumletea tija katika shughuli hiyo,na pia kuwa ni sehemu ya ajira hasa kwa vijana wazee walio katika umri wa kuustaafu hali itakayo wasaidia kujiingizia kipato na kuishi bila shaka yeyote ya kipato.
Kwa sasa samaki ambao hufugwa zaidi katika maji baridi (maji yasiyo ya chumvi) ambayo vyanzo vyake ni kama vile ya ziwa,mto,chemichemi ,kisima ya bomba,ni sato/pelage (Tilapia) na kambale (catfish).Kwa upande wa samaki wanaofugwa Zaidi katika maji chumvi(bahari) ni mwatiko/mkuyuyu (milk fish) na Kamba (prawns).
MWAKA HUU 2020 TUACHE UFUGAJI WA MAZOEA.

Monday, 25 February 2019

SOKO LA KAMBALE

Kambale ni aina ya Samaki anayefugwa kwenye maji baridi. Ni moja ya Samaki anayependwa sana ukanda wa Maziwa Makuu.

Kambale hupendwa sana sokoni akiwa amekaushwa kwa moshi au aliyechakatwa kwa kutengenezwa fillets.

Kwasasa Kambale anapata umaarufu wa kufugwa na wafugaji wengi kutokana na urahisi wa kumfuga, kwakuwa anakula vifaranga vya Samaki wengine na uhitaji wa kitoweo hasa akikaushwa.
Wasiliana nasi kwa huduma ya kukausha Kambale. 0784 455 683, 0673 455 683, 0753 749 992

Friday, 29 June 2018

CHANGAMOTO KUBWA TANO ZILIZOWAKUMBA WAFUGAJI SAMAKI.

Ufugaji wa samaki ni kazi ya kupanda,kukuza na kutunza samaki katika bwawa au uzio (uliotengenezwa kwa vyuma,miti pamoja na nyavu) au eneo lolote ambao uthibiti wake uko chini ya mamlaka ya mfugaji mwenyewe.Mabwawa yanaweza yakawa ya kuchimbwa na watu(japo kuwa mabwawa ya asili pia yanaweza kufugia samaki) wakati yale yanaweza yakawekwa katika eneo lolote lenye maji mengi kama vile ya ziwa,mto au bahari.

Ufugaji wa samaki katika kiasi fulani si sawa na ukuaji wa samaki katika mito,maziwa na bahari.Tofauti kubwa iliyopo samaki wanaofugwa na wasiofugwa ipo katika huduma,huduma wanazopata samaki wanaofugwa huwekwa kwa idadi maalumu ndani ya bwawa,kupatiwa chakula na kuhudumiwa vizuri.

Zifuatazo ni baadhi ya changamoto ambazo wameweza kukumbanazo wafugaji samaki

1.MABWAWA KUKUMBWA NA MAJI (MAFURUKO).

Hii ni moja changamoto kubwa sana iliyoweza kutokea katika kipindi cha mwezi wa watatu mpaka wa tano mwaka 2017,mabwawa haya yaliyokumbwa na mafuriko ni moja ya changamoto iliyotokea katika mabwawa ambayo yamechimbwa au kujengwa pasi kufuata taratibu za ujenzi au uchimbaji wa mabwawa,moja ya maeneo yaliyokumbwa na hali hii ni ruvu mkoa wa pwani,morogoro,mwanza,na mtwara hizi ni baadhi ya maeneo ambayo baadhi ya wafugaji wa samaki waliathirika na changamoto hii.

Sababu kuu inayopelekea mabwawa haya kukumbwa na mafurukio ni ujenzi usiozingatia tahadhari za kimazingira ikiwemo watu kujenga mabwawa kandokando ya ziwa,mifereji mikubwa na mabondeni,mara nyingi sana watu huchunguza eneo wakati ambao sio wa mvua hivyo kufikili ni maeneo salama kwao na kuanza kuchimba mabwawa.

Ushauri wa kitaalam kwa wafugaji wa samaki kuchukua tahadhari kubwa kabla ya kuanza ujenzi wa bwawa eneo lazima lifanyiwe uchunguzi wa kutosha kwa wakati wote kiangazi na masika ili kubaini eneo lako kama ni salama au sio salama ili kuepuka hasara zinazoweza kutokea,kuepuka kuchimba kando kando ya vyanzo vikuu vya maji kama vile kujenga bwawa kandokando ya ziwa,mifereji au kwenye mabonde kwani maeneo haya sio salama kwa ajili ya ufugaji wa samaki.

2. TATIZO LA MAADUI WA SAMAKI KAMA VILE NDEGE, KENGE, FISI MAJI NA NYOKA

changamoto hii uwepo wa ndege,kenge na fisi maji hupelekea kwa mfugaji kupata matokeo mabaya asiyoyatarajia kwa sababu samaki hupungua kwa kuliwa na maadui hao,mfano mfugaji anaweza akawa amepanda samaki 1000 hivyo hujikuta wakati wa mavuno samaki wanaopatikana ni 400 kati ya 1000 samaki wengine wameshambuliwa na hao maadui hao.

Sababu  za tatizo hili ni kujenga mabwawa sehemu zenye vichaka au kutovyeka majani kuzunguka bwawa la samaki hushawishi maadui hao kama vile kenge,nyoka na fisi maji huwa ni sehemu yao ya kujificha na baadhi ya mabwawa kutowekwa uzio na wavu wa juu kwa ajili ya kuthibiti maadui hao kupita na kushambulia samaki kirahisi.

Ushauri wa kitaalamu ni kuhakikisha eneo lako linakuwasafi halina kichaka na kuhakikisha kuweka uzio kuzunguka bwawa na kuweka  wavu juu ya bwawa kwa ajili ya kudhibiti ndege kutoingia ndani ya bwawa kirahisi.hivyo kufanya hivyo kunaongeza chachu ya mavuno chanya kwa mfugaji wa samaki.3.UGUMU WA KUKAUSHA MAJI BWAWANI.

Hii ni moja ya changamoto kubwa iliyobainika kwamba wafugaji waliowengi wamechimba mabwawa pasi kuweka mifumo rafiki wa kutolea maji,changamoto au athari kwa kutoweka mifumo ya maji hupelekea ubadilishwaji wa maji kuwa mgumu hali inayosababisha samaki kukaa na maji machafu kwenye mabwawa kwa muda mrefu,madhara makubwa ya maji machafu kukaa kwa muda mrefu kwenye mabwawa hupelekea samaki kukumbwa na magonjwa kama vile fungus au kufanya ukuaji hafifiu sana kwa samaki.

Tatizo hili la ugumu wa utoaji wa maji husababishwa na ujenzi wa mabwawa kutosimamiwa na wataalam husika wa miradii ya ufugaji samaki na mabwawa na pili husababishwa na bwawa

kujenjwa kwenye eneo la tambarare kiasi kuwa hakuna uwezekano wa kutumia bomba au kukata kuta za bwawa kuondoa maji.

Utatuzi wa tatizo hili ni kuhakikisha kuwa unafuata kanuni zote muhimu za uchimbaji wa mabwawa ikiwemo mfumo wa kutolea maji,unachimba bwawa kwa kuzingatia sehemu yenye mwinuko wastani ili kupata mlalo halisi utakao tililisha maji yote kutoka bwawani na kufanya ufugaji mzuri unazingatia kanuni bora za ufugaji samaki wenye tija.4.KUIBUKA KWA UGONJWA WA KUPASUKA KICHWA KWA SAMAKI TATIZO HILO LIMEIBUKA ZAIDI HUSUSANI KWA WAFUGAJI WA KAMBALE.(CRACK HEAD DISEASE IN CATFISH).

Hii ni moja ya changamoto iliyowakumba baadhi ya wafugaji wa samaki kwa msimu uliopita,tatizo hili limelipotiwa na baadhi ya wafugaji hususani wenye mabwawa ya kujengea kwa tofali,baada ya kuona samaki wao wanakufa hususani kambale,kupitia jarida hili la mkulima mbunifu wafugaji kadhaa walioripoti taarifa hizi kwa mtaalam wa samaki alifika na kubaini tatizo hili moja kwamoja kutoka kwa wafugaji,moja ya dalili za ugonjwa huu samaki huanza kwa vilia damu sehemu za juu ya kichwa chake kisha hupasuka na kutengeneza kidonda ambacho huanza kuwa kidogo kisha hukua na baadae hupelekea kifo cha samaki.,

Tatizo hili husababishwa zaidi na ukosefu au upungufu wa baadhi ya virutubisho,moja ya virutubisho hivyo muhimu kwa kambale kuvipata ni vitamin C,uwepo wa vitamin hii humfanya kuimalisha mwili wake na kufanya utengemavu mzuri kwenye mfumo mzima wa mifupa yake,ni hii hutokana sana na ulishaji usiozingatia kanuni bora za utengezaji wa chakula cha samaki kulingana na samaki husika ,hivyo hupelekea kutokea kwa tatizo hilo la kupasuka kwenye sehemu ya mwili wake.

Ushauri wa kitaalam unapoona tatizo hili limetokea haraka sana wacha kutumia chakula ambacho hicho ndio kimepelekea kutokea kwa tatizo hilo,tengeneza chakula au lisha chakula chenye virutubisho vya vitamin C  na amino acid  kwa ajili ya kurejesha hali ya samaki kwenye afya yake,kama tatizo hili litaendelea ni vema sana kupata ushauri wa wataalam wa samaki kwa ushauri wa kina zaidi.

5.WAFUGAJI WENGI KUTOKUWA NA USIMAMIZI MZURI KWENYE MIRADI YAO.

Mradi wowote ili ukue vizuri tunahitaji sana uwepo wa usimamizi mzuri wa mradi huu wa samaki ambao unatija zaidi kwa jamii,moja ya changamoto kubwa sana ambayo imejitokeza zaidi ikiwemo na hii ya usimamizi hafifu kwenye mradi,tunapo sema usimamizi hafifu hapa tuna maanisha kwamba baadhi ya wafugaji wengi wamepata matokeo ambayo sio ya kulidhisha kwenye mavuno yao kwa sababu hakuna uwekaji wa kumbukumbu yeyote ile kuanzia siku ya kuchimba bwawa,kuweka samaki,ulishaji wa samaki na malipo ya vibarua,uwekaji wa kumbukumbu ni moja ya vitu muhimu sana kwenye mradi ambayo itakusaidia wewe kufahamu kuwa umetumia kiasi gani na baada ya mavuno kufahamu umeingiza kiasi gani,baadhi ya wafugaji wamekuwa hawalisha chakula kwa wakati uliopangwa,kutobadilisha maji pindi yanapokuwa yamechafuka,na kutofanya usafi nje ya bwawa hali inayopelekea kukarisha maadui wa samaki kama vile kenge,fisimaji, na nyoka.

Ushauri wa kitaalam ni vema sasa wafugaji kufuata nakuzingatia kanuni zote za ufugaji ikiwemo ulishaji kwa wakati kwa samaki,ubadirishaji wa maji na usafi nje ya bwawa kwa ajili ya usalama ambayo itapelekea kupata matokeo chanya zaidi na kufurahia biashara hii yaufugaji wa samaki.

Hayo ndio changamoto kuu tano zilizowakuta wafugaji wa samaki kwa msimu wa mwaka 2017 hivyo ni vyema sasa mfugaji wa samaki kuzingatia na kuepuka changamoto ambazo zinawezakujitoeza.

Tuesday, 12 June 2018

TEKNOLOJIA MPYA YA UFUGAJI WA SAMAKI KWA NJIA YA MABWAWA YA PLASTIKI

HATUA ZA AWALI ZA UANDAAJI WA BWAWA LA PLASTIKI TAYALI KWA KUPANDA SAMAKI NJIA HII ITASAIDIA WENGI HASA WAISHIO MIJINI .

UTAMBUZI WA UWEKAJI WA SAMAKI KWENYE BWAWA.


Wafugaj wengi sana huwa na maswali meng juu ya ufahamu  ni kiasi gani anapaswa kupandikiza kwenye bwawa lake baada ya ujenzi na hatua zote muhimu kukamilika ikiwemo ujuzaj iwa maji.

Ni muhimu sana kwa mfugaji kufamu anahitajika kuweka samaki kasi gani kwenye bwawa lake ili aweze kupata matokeo chanya kwa samaki na wakuwe katika muda husika .

Katika ufugaji wa samaki ndani ya bwawa ya samaki huwekwa kwa idadi maalum ndani  ya mita moja ya mraba,uwekaj huu wa dad ndo hutofautisha aina za ufugaji samaki,ambao huita ufugaji mdogo,ufugaji wa kati na ufugaji mkubwa.Endapo mufugaji asipozinngatia kanuni hizo za uwekaji wa samaki kwa idadi maalum basi hupelekea mfugaji kuona shughuli ya ufugaji samaki ni mradi usio na tija kwake.

Uwekaji wa samaki kwenye bwawa huwekwa kwa idadi maalum kawaida/kitaalam mita moja ya mraba unaweza kupandikiza samaki kuanzia 3-5,6-10,11-15,16-30.mfano bwawa likiwa la mita 30 x mita 20= mita za mraba 600 x samaki 5=samaki 3,000.

Idadi hii samaki huwekwa kutokana sababu zifuatazo ambazo hupelekea kufanya maamuzi ya kuweka samaki kutoka 3-30.

1.upatikanaji wa maji ya kutosha na uhakika.

2.uwezo wa uhakika wa kulisha samaki wako kwa kipindi chote cha ufugaji.

1.UPATIKANAJI WA MAJI YA KUTOSHA NA UHAKIKA.

Wafugaji wengi hutamani sana kuweka samaki kwenye dogo pasi kuangalia idadi hiyo ya samaki bwawa alilonalo na chanzo cha maji haviendani,kwa mfano unabwawa lenye ukubwa wa mita 2 kwa mita 3 ambalo jumla za mita eneo sita alafu mfugaji anataka kuweka samaki 500 au 1000,chanzo cha maji ni kisima ambacho hakitoi maji ya uhakika kwa muda yanapohitajika pindi yanapochafuka.

Kigezo cha maji husaidia mfugaji kujua endapo anaweka samaki wengi anauwezekano mkubwa sana wa kubadilisha maji muda wowote bila shaka yeyote ile,uwepo samaki wa samaki kwenye bwawa hupelekea maji kuchafuka kwa haraka sana kupelekea harufu ya maji na mwisho hupelekea samaki kukosa hewa na kufa kitu ambacho huleta hasara kwa mfugaji husika.

Maji ya uhakika ambayo hupelelea mufugaji kupandikiza samaki wengi katika eneo dogo ni kama vile maji ya chemichemi,maji yanayotiririka kutoka milimani,mifereji ya maji safi na salama ambayo hutiririsha maji wote,maji ya mto,ziwa au mababwa makubwa,hivi ni mojawapo ya vyanzo vya maji ambavyo mfugaji alichimba bwawa/mabwawa karibu na vyanzo hivi uwekaji wake wa samaki huwa kulinganisha na mfugaji aliyembali na vyanzo hivi ikiwemo wanaotumia maji ya visima au maji ya bomba.Endapo mfugaji kwa kushirikiana na mtalaam watajilidhisha chanzo chao cha maji ni ya uhakika basi wanaweza kufuga samaki wengi kwenye eneo dogo.

Maji ambayo sio ya uhakika na sio vema sana ni kama vile maji ya visima,maji haya hutumia nishati ya umeme ili yatoke,endapo mfugaji ataweka samaki wengi kuliko chanzo chake kitamlazimu kubadili maji mara kwa mara hali ambayo hupunguza faida katika ufugaji kwa kuongezeka kwa gharama za maji,vyanzo vingine ni kam vile maji ya bomba ( DAWASCO) maji ya mvua na kununua kwenye madumu.

Endapo mfugaji atalazimika kuweka samaki wengi atalazimika kutumia mitambo maalum ya kuongeza hewa na kuchuja uchafu,ili kufanya ubora wa maji wa kuwa katika ubora kwa muda mrefu bila kubadirisha maji,wafugaji katika matumizi ya mitambo huwa na umeme wa uhakika muda wote,ufugaji huu huitwa mfugaji mkubwa,ambao wafugaji wadogo ni vigumu kugharamia mfumo hivyo huweka samaki ambao ana

ZINGATIA.Maisha ya samaki yeyote Yule ni maji,hewa anatumia inatoka kwenye maji hivyo uchafukaji wa maji hupelekea samaki kushindwa kupumua vizuri  hali inayopelekea ukuaji hafifu au vifo kwa samaki.

MUHIMU.ni muhimu sana kupima maji yako kabla ya kuanza ufugaji samaki,na baada ya kuanza ufugaji ili kufamu maji yako yaposalama kiasi gani,usisubili mpaka maji yatoe harufu ndipo ubadilishe maji.

2. UWEZO WA UHAKIKA WA KULISHA SAMAKI WAKO CHAKULA KWA KIPINDI CHOTE CHA UFUGAJI.

Hii ni sehemu ya pili muhimu katika utambuzi wa uwekaji wa samaki kwenye bwawa lako,baada ya kujiridhisha kwamba chanzo changu cha maji yanafaa kufugia samaki ni vema sana kufanya tathimini ya samaki wako wanakula kiasi gani kwa kipindi chote cha ufugaji,mfano unataka kufuga samaki 1000 kipindi cha ufugaji ni miezi 6,samaki 1000 watakula kilo 90 bei ya kilo shilingi 2000 jumla ya gharama ni shilingi 180,000.Baada ya kufanya tathimini ya gharama hizo utakuwa na maamuzi sahihi kuwa unaweza kuhudumia samaki hao kwa kipindi chote hicho au hapana,maamuzi hayo yanaweza kukusaidia kuongeza au kupunguza idadi.Moja ya dosari ambazo hujitokeza ni kulisha sana miezi miwili au mitatu ya mwanzo miezi mingine mfugaji hushindwa kuhudumia chakula hali ambayo hupelekea samaki kudumaa au kutokuwa vizuri katika uzito unaohitajikaFAIDA YA KUWEKA SAMAKI KWA IDADI MAALUM KWENYE BWAWA .

1.samaki hukua kwa haraka

2.maji kutochafuka kwa haraka bwawani.

3.kuepuka magonjwa ya samaki

4.samaki kutodumaa au kufa.

HASARA YA KUTOWEKA SAMAKI KWA IDADI MAALUM.

1.maji huchafuka haraka.

2.samaki kutokuwa vizuri.

3.samaki kupata magonjwa /kufa.

Nukuu.hakuna athari yeyote endapo mfugaji ataweka samaki wachache kwenye bwawa lake.

Thursday, 14 December 2017

HABARI NJEMA KWA WAFUGAJI SAMAKI KWA KUPATA TAASISI YA KUWATETEA(AQUACULTURE ASSOCIATION OF TANZANIA (AAT).

Pongezi kubwa sana ziwafikie waratibu wote waliofanikisha zoezi hili la kukamilika kwa usajili wa taasisi ambayo itasaidia kusonga mbele kwa shughuli nzima zinazohusu kilimo maji.
AQUACULTURE ASSOCIATION OF TANZANIA (AAT) ni taasisi ambayo kwa kiasi kubwa itasaidia kuwatambua wataalam wanaosimamia shughuli hizi tofauti na ilivyo sasaivi kila mtu anakuwa mfugaji kisha kuwa mtaalam na kueneza taaluma kwa wengine pasi kufuata utaratibu na kanuni za kilimo maji nchini jambo ambalo kwa kiasi kikubwa kimewakwamisha baadhi ya wafugaji kufikia malengo yao kwa sababu za wasimamizi wasio na sifa za kufanya kazi za kitaalam za ufugaji samaki.
AAT Itasaidia zaidi kupunguza mzigo mkubwa kwa serikali katika kusimamia kanuni na sheria juu mambo mbalimbali yanayotokea kwa wafugaji na watendaji wengine.
AQUES LTD Inapongeza sana kwa wote waliohusika katika mchakato mzima wa kukamilika kwa taasisi iliyosajiliwa kisheria na kupewa usajili nambari S.A.20925 kwa mujibu wa sheria za taasisi (CAP.337 R.E.2002)
Hivyo shime kwa wafugaji samaki kama sehemu yao salama katika utekelezaji wa miradi yao ili kufikia mafanikio.

Wednesday, 13 December 2017

HATUA KUMI MUHIMU ZA UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA SAMAKI
1.      Kusanya malighafi zinazohitajika kwa ajili ya utengenezaji wa chakula.

2.      Kausha mazao yote mpakayaweze kusagika au kutwangika kirahisi.

3.      Pima uzito unaotakiwa kulingana na muongozo na utengenezaji wa chakula.

4.      Saga na twanga mchanginyiko huo uwe kwenye hali ya ungaunga (powder form).

5.      Changanya mchanganyiko wako vema na kasha weka maji kiasi chakula kiwe kwenye hali ya majimaji ya wastani.

6.      Ingiza kwenye mashine ya kutolea chakula hicho kiweze kutokea mithili ya tambi (peletting machine).

7.      Anika chakula chako sehemu yenye kivule mpaka kikauke vizuri.

8.      Anua/toa chakula chako na kuhifadhi vizuri chakula sehemu pakavu na salama

9.      Lisha asilimia 5-10 ya uzito wake.

10.  Kama hujui uzito wa samaki wako wape chakula kidogokidogo mpaka waache kula kama dalili ya kuwa wameshiba,hivyo endelea kufanya kwa muda na hatimaye kujua samaki wako wanakula kiasi gani.

11.  Tunashauri mfugaji ulishe samaki wako sehemu moja tu ya bwawa lako,kwa muda wa  asubuhi (saa 2-4) na jioni (10-12).Usibadilishe badilishe sehemu ya kulisha chakula na pia usizidishe kiwango cha ulishaji kwa samaki.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa