Thursday, 10 July 2014

JE UNAFAHAMU JINSI YA KUPATA CHAKULA BORA CHENYE RISHE KWA SAMAKI?

MUONGOZO WA JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI (ARTIFICIAL FEED) SATO (PELEGE).
Jinsi ya kuweza kupata au kutengeneza  chakula kilichobeba  virutubisho vyote  muhimu ya vyakula  mjumuisho wa virutubisho  muhimu ambavyo vitasaidia samaki katika ukuaji wake  mzuri bila matatizo. Hakikisha  chakula unachotengeneza  kinakuwa na virutubisho vifuatavyo  ili uweze kufahamu vyema ni vitu gani  ambavyo vinabeba virutubisho hivyo:
·         Protein, ( kiini rishe)
·         Carbohydrate  (wanga)
·         Fat /lipid (mafuta)
·         Vitamin (vitamin)
·         Minerals (madini)

·         Viritubisho hivyo vitano ni muhimu  kwa samaki kwa sababu  kila moja ina kazi yake ndani ya mwili wa samaki  husika ambaye anafugwa.
·         Chakula cha samaki hutengenezwa  kulingana na aina ya samaki husika : mfano  samaki aina ya  Nile Tilapia (sato, pelage) Grouper (cehewa) mwatiko ( milk fish) Cat fish (kambale)  mchanganyiko wake huwa tofauti tofauti
·         Muongozo huu ni maalumu  ni kwa ajili ya samaki aina  Tilapia (sato, pelage)
MAHITAJI
v  Fish meal ( unga wa dagaa) protini ya mnyama
Uwe umesagwa  kwenye hali ya ungaunga   (powder form ) kazi kubwa ya protein  hii ni kufanya mwili kukua vizuri ,protini hii huitajika kwa wingi zaidi hasa kipindi ambacho samaki huwa mdogo na katika lika la samaki mzazi.
v  soya bean(soya lishe) protini ya mmea
hii nayo ni aina protini ambayo hufanya kazi ya kuimalisha mwili na kukua kwa samaki vizuri,pi protini hupayikana katika mimea jamii ya mikunde,unachemsha kidogo,unazianika mpaka zikauke alafu unazizaga ili ziwe kwenye hali ya unga unga,hutumika kwa wingi katika cha samaki anapo kuwa mdogo sana kipindi anachofikia kuwa mzazi(broder fish)
v  rice bran,maize bran (pumba za mpunga,pumba za mahindi).
Hiki ni chakula jamii ya wanga (carbohydrate) ambayo hufanya kazi ya kuongeza nguvu ndani ya mwili wa samaki,pumba lazima ziwe zimesagwa vizuri na  kuwa katika hali ya unga unga ili kumpa nafuu samaki katika ulaji wake,huchanganjwa zaidi kipindi ambacho samaki yupo katika lika la kati (grow out).tunapendekeza sana kuanza kutumia pumba za mpunga ni nzuri zaidi ila kama hazipatikani unaweza pia kutumia pumba za mahindi
v  Cassava flour,wheat flour (unga wa mhogo,unga wa ngano)
Hii nayo ni aina mojawapo ya chakula aina wanga ambayo husaidia katika kumpa samaki nguvu  ndani ya mwili wake,kazi nyingine husaidia kuviunganisha virutubisho vyote kuwa kwenye sehemu moja (single compound) hivyo humfanya samaki kula virutubisho vyote kwa wakati moja,tunapendekeza kuanza kutumia unga wa mhogo ila kama haupatikani basi unaweza kutumia unga wa ngano.
v  Copra meal,sun flower cake (machicha ya nazi,mashudu ya alizeti).
Hii ni aina mojawapo ya virutubisho aina ya mafuta ambayo hufanya kazi ya kunenepesha mwili wa samaki vizuri.
v  Vitamin mineral mix,premix and D.I GROW .
Hivi ni aina za vitamin na madini ambayo hufanya kazi ya kuimarisha mifupa na kulinda mwili wa samaki kwa ujumla dhidi ya magonjwa na mashambulio mengine,endepo vitamin mineral haipatikani katika mazingira yako unaweza kutumia premix ya kuku wa kisasa ya kukuzia kwa ya kukuzia samaki wako kwa sababu vitamin na madini yake yanafanana katika utengenezaji wa chakula,na hiyo pia kama haipatikani unaweza pia kutumia D.I GROW kwa ajilia ya kutengenezea chakula chako.
KIWANGO KINACHOHITAJIKA KATIKA UCHANGANYAJI WA CHAKULA CHA SAMAKI AINA YA NILE TILAPIA.
KANUNI (namba ziko katika asilimia)
1.UNGA WADAGAA=18.25
2.SOYA LISHE=25
3.PUMBA ZA MPUNGA/MAHINDI=36.42
4.MACHICHA YA NAZI,MASHUDU YA ALIZETI=10
5.UNGA WA MHOGO/NGANO=6
6.VITAMIN MINERAL MIX,PREMIX AND D.I GROW=4.33
MFANO TUNATENGENEZA CHAKULA CHA SAMAKI CHA KILO HAMSINI (50 KG).
*namba ya 50,000 kilo ambazo zipokwenye gram hivyo zimebadilishwa kuwa kwenye kilogram.
1.Unga wa dagaa :18.25÷100×50,000=9.125 kg
2.soya lishe:25÷100×50,000=12.5 kg
3.pumba za mpunga/mahindi:36.42÷100×50,000=18.21
4.unga wa mhogo/ngano:6÷100×50,000=3kg
5.machicha ya nazi,mashudu ya alizeti:10÷100×50,000=5kg
6.vitamin mineral mix,premix.D.I GROW:4.33÷100×50,000=2.165kg
7.mchanganyiko huo huchanganjwa na maji nusu ya uzito wa chakula,mfano chakula unachotengeneza kilo 50 changanya na maji lita 25.
*lakini maji unaweza kuongeza maji endapo mchanganyiko wako bado ni mkavu sana,na pia unaweza kuanza kuweka maji taratibu mpaka pale utakapo ona mchanganyiko wako unakuwa unashikana shikana,mchanganyiko usiwe na maji mengi sana na usiwe na maji kidogo sana yawe ya wastani.
*usianike chakula chako kwenye jua unapoteza virutubisho vyako katika njia ya mvuke,anika kivulini ili zikauke na upepo.
*hifadhi chakula chako mahali salama ili kisiweze kuoza na kutoa fangasi au ukungu mweupe ambao hutokea kwenye chakula samaki.
*endapo unahitaji kutengeneza chakula  kidogo yaani mfano wake unataka kutengeneza chakula cha kilo 25 basi unagawa kwa mbili,machicha ya nazi kilo 5 basi una gawa kwa 2,(2÷5)=2.5kg hivyo chakula cha kilo 25 unaweka machicha ya nazi kilo 2.5
*endapo unahitaji kutengeneza chakula kingi zaidi basi unazidisha mara mbili yake mfano unataka kutengeneza chakula cha kilo 100.pumba za mpunga kwa kilo 50 unaweka kilo 18.21 je kilo 100 naweka kiasi gani?unazidisha mara mbili 18.21 ×2=36.48.hivyo unajua chakula cha kilo 100 unaweka pumba za mpunga kilo 36.48.
*lishia samaki wako chakula hiki mara mbili kwa siku asubuhi katika hali ambayo kiwango cha jua hakijawa kikubwa na jioni juu linapokuwa limepungua.
*kiwango cha kulishia samaki wako njia rahisi ni siku mbili za mwanzo ndizo zitatoa majibu samaki wako wanahitaji kula kiasi gani,kama siku ya kwanza uliweka kiwango kadhaa wakabakisha basi kesho yake punguza kipimo mpaka uone sasa chakula unachowapa kinawatosha na hawabakishi.
MWISHO
MUONGOZO HUU WA CHAKULA SAMAKI UMEANDALIWA NA AFISA MRADI-UWASA.
MUSA SAIDI NGAMETWA
Kwa maswali au ushauri wasiliana   nami kwa mawasiliano yafuatayo
Cont:0718 98 63 28
0686 47 93 48

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa