Monday, 21 July 2014

MAJIBU YA MASWALI UNAYOJIULIZA MFUGAJI WA SAMAKI....

SWALI LA KWANZA
Naweza kujenga bwawa dogo kwa kutumia tofali likashabihiana na dirisha la nyumba yangu?
JIBU
Ndio inawezekana kujenga bwawa dogo tu kando kando ya nyumba kikubwa ni kizingatia mzingi wa nyumba yako kuwa ni imara na ardhi uliyopo haiwezi kuleti ufa,hiyo nyia pia ni moja ya wapo kama pambo la nyumba kwani mfano wake ni kama vile umetengeneza bustani ila sasa bustani yako wewe ni ya kujenga bwawa na kupandikiza samaki.mfumo huu pia hutumiwa zaidi na watu nchini zinazo ongoza kwa ufugaji kama vile misri,ifilipino na china.
kutumia maji ya bomba katika ufugaji wa samaki ni sawa kikubwa ni kuhakikisha maji hayo ni safi na salama katika ufugaji wa samaki,pia unaweza kutumia maji ya mto,mifereji iliyo salama na maziwa,kikubwa kushirikisha wataalamu katika hatua kama hiyo muhimu kwani maji huwezi kuyakagua kwa kuyaangalia tu.
SWALI LA PILI.
Naweza kutengeneza chakula samaki kuwa kama tambi au vipunje vidogo vidogo?
JIBU.
Futilia muuongozo wa utengenezaji wa chakula katika blog hii hii nimeeleza vizuri sana katika utengeneza wa chakula,ili uweza kutengeneza chakula hiki kiwe katika mfumo huo unahitajika uwe na mashine mfano kama ile ya nyama pellete ili iweze kutokea katika mfumo wa tambi.

mashine hiyo ndogo husaidia kutoa chakula cha samaki katika mfumo wa tambi ambao husaidia samaki kula chakula ambacho kimebeba virutubisho vyote muhimu.

chakula cha samaki kilicho tayari kutengenezwa na kuanikwa kivuli tayari kwa kuanuliwa na kulishiwa kwa samaki,chakula hiki hulishwa samaki wakubwa,samaki wadogo hulishwa chakula kilicho katika hali ya unga kulingana na ukubwa wa midomo yao.chakula hiki hakipaswi kuanikwa juani kwani kitapoteza virutubisho vyote muhimu kwa njia ya mvuke wa jua.huu ni moja tu ya mfano wa chakula kwa samaki wanakuwa,chakula hiki hutengenezwa kulingana na ukubwa wa samaki,samaki mdogo anakiwango chake,wa kati na mkubwa pia anakiwango chake.
wasiliana na mtaalamu kwa maelezo zaidi.
kuchanganya uwiano tofauti wa chakula utapelekea chakula kuto kuwa na virutubisho vizuri kwa ajili ya kukuza samaki wako.
0718 986328.
0686479348.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa