Monday, 28 July 2014

MFUGAJI JENGA TABIA YA KUSHIRIKISHA WATAALAMU WA SAMAKI KABLA YA KUANZA MRADI NA BAADA YA KUANZA MRADI.

tembelea blog hii na utaunganishwa na wataalamu popote pale ulipo.Ndugu mfugaji,uliye anza kufuga ama uko njia kuingia katika mradi wa ufugaji wa samaki ni kosa kubwa sana ambalo wafugaji wa samaki hulifanya la kutoshirikisha wataalamu katika hatua ya awalu eidha kwa kukwepa gharama kutowapata wataalamu kirahi au la.Mfano utakuta mfugaji ana anza kuchimba bwawa la samaki kwa kupitia maelezo katika mtandao,jamani siku zote nadhalia huwa hazifanani na vitendo,nadhalia huwa haibadiliki kama ulisoma kitu sehemu fulani,lakini kujifunza kwa matendo huwa ni vema na utajuwa na wa kubadilisha au kuongeza katika shughuli zako,sasa mfugaji huyo kwa kusoma tu utakuta ameridhika na kuanza kutafuta vibarua wa kuchimba,kujaza maji na baadae kujaza samaki katika mabwawa.Kikubwa ambacho nahitaji kueleza hapa ni kwamba ni muhimu sana hatua ya awali kumpata mtaalamu  kwenda nae mpaka kwenye eneo husika  unalotaka kufanyia mradi wa samaki.Yeye ndie atakushauri kulingana na mazingira na tabia ya hilo eneo.Kutofanya hivyo nikujikuta unaingia katika gharama kubwa sana kwa kufanya mwenyewe tofauti kumshirikisha mtaalamu kujua namna ya kupunguza gharama.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa