Monday, 21 July 2014

NAJIVUNIA FAIDA YA UFUGAJI SAMAKI.HADITHI YA KWELI.

Bwana said bakari ni moja wa wafugaji wa samaki aina ya mwatiko katika kijiji cha namindondi kilichopo wilaya Mtwara vijijini, haikuwa kazi rahisi kwa upande wake kuweza kukikidhi mahitaji yote yaliyokuwa yanahitajika kwenye shughuli nzima ya ufugaji wa samaki, alianza ufugaji wa samaki kutoka na kupata ushawishi wa kupitia mabwawa ya chumvi, wakati wakiwa wanazalisha chumvi huingia na samaki ambao walikaa kwa muda na kukuwa hivyo ushawishi wa kuanza kufuga samaki ulipoanza, aliamua kuanzisha kikundi kwa mara ya kwanza cha ujasiliamali kinacho jihusisha na ufugaji wa samaki, wanakikundi wengi wakakata tama kutoka nan a  kutoona mafanikio yeyote katika ufugaji wa samaki kwani walianza ufugaji pasi kuwa na taaluma yeyote juu ya ufugaji wa samaki lakini pia  kutokana na sababu na changamoto zilizojitokeza kwenye kikundi ikiwemo ushiriki mdogo wa watu katika kazi ikapeleke kikundi  hicho kuvunjika. Bwana Saidi Bakari hakukata tama aliamini siku moja atapata mafanikio makubwa kupitia ufugaji wa samaki, alifanikiwa kuanzisha kikundi cha watu sita mwaka 2011 lakini kati ya hao moja wapo akajitoa na kufikia watu watano ambao wapo mpaka sasa, kikundi chao walikipa jina la mapambano, mnamo mwaka 2011 waliweza kukamilisha bwawa lenye eneo la mita za mraba 5600, baada ya kukamilisha ujenzi waliweza kupandikiza vifaranga vya samaki aina ya mwatiko wapatao 10,000 walifanikiwa kuvuna samaki wote lakini matokeo yake hayakuwa mazuri kwa sababu samaki hawakukuwa hii ilisababiswa na  kutokuwa na  elimu  juu ya ufugaji wa samaki, walifanikiwa kupata kipato cha shilingi 300,000 waligawana 60,000 kwa kila moja kwa watu watano.  Mwaka 2012 walifanikiwa kujiunga na shirika la UWASA umoja wa wafugaji samaki Mtwara, na waliweza kupatiwa elimu ya ufugaji endelevu wa samaki na pia walipatia  fedha kwa ajili ya kuboresha bwawa na  ujenzi  wa  geti   kwa ajili ya kutolea maji na kuingiza maji, pia waliweza kupatiwa  chakula cha kulisha samaki. Mwaka 2011-2012 walipandikiza vifaranga 10,000 na kufanikiwa kuvuna samaki 8876  na kupata fedha tasilim sh 4,962,000/=  ( milioni nne laki tisa sitini na mbili elfu tu ) na waliweza kugawana   400,000 ( laki nne)  kwa kila moja ,  mavuno ya mwaka,  2013 waliweka samaki  8,000   na kuvuna samaki 6754  na kupata kiasi cha Tsh 1,107, 000   kutokana  na mavuno ya 2012 na 2013 na elimu aliyoipata bwana Said Bakari amefanikiwa kukarabati nyumba kwa kuweka  bati, umeme, kununu jokofu,  na televisheni ya kisasa na kufanikiwa kuongeza kipato kwa kujiongezea mtaji kwenye shughuli zake za kilimo na biashara “ maisha yangu yamebadilika  kutokana  na shughuli ninazozifanya za  ufugaji wa samaki   na kujiongezea mtaji katika  kilimo na biashara ’’ .

Baadhi ya picha ya vitu vya thamani anavyomiliki bwana Saidi Bakari,akijivunia moja ya mafanikio katika ufugaji wa samaki.Pia anajinasibu kwa kusema kwamba amejipanga kwa kuleta mafanikio kwake na kusaidia jamii ya kijiji chake kuwekeza katika ufugaji wa samaki,pia alilisitiza kwamba mafanikio ya hivi karibuni kuendelea kushilikisha wataalamu katika shughuli zake.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa