Monday, 14 July 2014

JE?UNAFAHAMU SAMAKI ANAFUGWA VIPI?muongozo wa UFUGAJI WA samaki na FAIDA ZAKE
Ufugaji samaki ni kazi ya kupanda,kukuza na kutunza samaki katika mabwawa,mito au maziwa. Mabwawa yaweza kuwa ni ya kuchimbwa na watu (japokuwa ya asili pia huweza kutumika) wakati uzo inaweza ikawa imewekwa  katika eneo lolote lililo na maji kama ziwa na hata bahari.
Ufugaji samaki kwa kiasi fulani si sawa na ufugaji samaki katika mito, maziwa na bahari. Tofauti iko katika huduma inayotolewa kwa samaki wafugwao na idadi ya samaki wanaopaswa kuwamo ndani ya eneo husika. Samaki wanaofugwa huitaji kulishwa na kuhudumiwa.
Ufugaji wa samaki si kitu kipya kabisa hapa Tanzania. Baadhi ya watanzania wamekuwa wakifuga samaki katika mabwawa hata kabla ya nchi yetu kupata uhuru.Lakini baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitoa matunzo hafifu kiasi cha kufanya mavuno kutokuwa mazuri. Kwa miaka ya karibuni, serikali imetilia mkazo utoaji elimu (ugani) wa ufugaji samaki ili kuboresha mafanikio yake. Kuchapishwa kwa chapisho hili litasaidia kuongeza uelewa kwa wafugaji samaki katika shughuli nzima ya ufugaji samaki nchini.
FAIDA ZA UFUGAJI WA SAMAKI
Ufugaji samaki unafaida nyingi sana, baadhi hizo ni kama hizi hapa chache ambazo nimeweza kuziainisha.

 •         I.            Kujipatia kipato baada ya kuuza samaki waliofugwa.
 •       II.            Kuboresha kazi nyingine za kilimo kama bustani ya mboga , ufugaji wa ng’ombe, bata, kuku, nguruwe bustani ya miti n.k.(ufugaji wa samaki hupelekea kufanya shughuli nyingine za kilimo na ufugaji mwingine kwa wakati mmoja).
 •     III.            Ufugaji wa samaki husaidia kutumia ardhi ambayo isingeweza kutumika katika shughuli nyingine za uzalishaji mali.
 •     IV.            Eneo la bwawa huwa ni sehemu mzuri ya mapumziko.
 •       V.            Ufugaji wa samaki husaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa.
 •     VI.            Ufugaji wa samaki hutumika kama pambo ndani ya nyumba,katika migahawa na mahoteli.
 •   VII.            Kuongeza rishe mwilini kwa kiasi kikubwa.
 • VIII.            Husaidia kutunza na kuhifadhi jamii za samaki ambazo ziko mbioni kutoweka.

HATUA MUHIMU KATIKA SHUGHULI YA UFUGAJI WA SAMAKI
        i.            Uchaguzi wa mahala panapofaa kwa ajili ya kuchimba bwawa la samaki:

 • i.Fanya udadisi kwa kushirikisha wataalamu wa fani ya ufugaji wa samaki na kukushauri endepo eneo lako linafaa kwa ufugaji wa samaki halifai.
 •       ii.            Tathimini ya umbo na ukubwa wa bwawa kulingana na eneo ulilinalo,kiwango cha fedha ulichonacho kwa ajili ya kuanza mradi.
 •     iii.            Uchimbaji wa bwawa.
 •      iv.            Uingizaji na uotoaji wa maji katika bwawa
 •        v.            Uwekaji wa mbolea na majivu au chokaa,hii itasaidia kurutubisha bwawa lako kwa ajili ya kutengeneza chakula cha asili ndani ya bwawa.
 •      vi.            Upandaji wa vifaranga vya samaki
 •    vii.            Ulishaji wa samaki na matunzo mengine  bwawani
 •  viii.            Uvuaji wa samaki na aina ya nyavul/ zana zifaazo kutumika..


VIGEZO MUHIMU KWA KUBORESHA ULISHAJI

 •         i.            Joto au ubaridi wa maji katika sehemu husika huweza kuongeza au kupunguza hamu ya ulaji wa samki na hivyo ukuaji wake.
 •       ii.            Chakula cha samaki (cha asili na cha ziada ), aina ya vhakula na kiasi kinachopatikana.
 •     iii.            Uwingi wa samaki waliopo bwawani kulinganisha na ukubwa wa bwawa.
 •      iv.    Ubora wa vifaranga(quality) waliopandwa. Vifaranga wenye ubora mzuri huwa na uwezo wa kukua haraka.
 •        v.            Muda uliotumika kuzalisha  samaki. Japokuwa samaki hukuwa haraka wanaitaji muda wa kutosha kufikia ukubwa unaofaa kwa mahitaji ya mkulima au wa soko.
 •      vi.            Uwepo wa magugu na mimea isiyohitajka bwawani.
 •    vii.            Uwepo wa maadui wa samaki ( predators.)
 •  viii.            Kuwa na tabia ya kuvua bwawa kila baada ya miezi 6 hadi 9 kwa kulikausha ili kuboresha mazngira yake .
 •      ix.            Huduma inayotolewa bwawani usaidia kupatikana samaki wakubwa  na wenye afya.

UCHAGUZI WA ENEO LA KUCHIMBA  MABWAWA NA UINGIZAJI WA MAJI KWENYE BWAWA
1.ni jambo muhimu sana kuchagua eneo zuri ili kurahisha na kufanikisha kwa urahisi kazi ya kufuga samaki.
2.si kila eneo hufaa kufanya kazi ya ufugaji samaki.
3.eneo zuri kwa ufugaji wa samaki ni eneo lenye maji ya kutosha na ya kuaminika,udongo unaotuamisha maji (mfinyanzi),ikiwezekana kuwa na mtelemko kiasi,eneo kama halina udongo wa mfinyanzi lakini maji ya kutosha yanapatikana kwa wingi unaweza kufuga samaki kwa kujenga bwawa kwa kutumia simenti.
4.maji ya kutosha ni yale yanayoweza kujaa kwenye bwawa lako katika kiwango kinacho takiwa kuanzia mita moja mpaka mita moja na nusu,vyanzo vya maji ambayo unaweza kutumia ni kama vile ya mto,ziwa au chemichemi ambayo nayo lazima yawe safi na salama katika ufugaji wa samaki.
5.udongo unafaa ni ule wa unaotuamisha maji kwa muda mrefu,kama vile wa mfinyanzi au mchanganyiko wa mfinyanzi na tifutifu.mchanga mtupu haufai kwani huruhusu maji kunywea kirahisi.

vitu muhimu vya  kuzingatia katika ulishaJI samaki
1.      Samaki ni viumbe ambao maisha yao hutegemea maji katika kuishi.Ulaji wao mzuri unategemeana na vipindi mbali mbali vya hali ya hewa hususani katika hali ya joto la wastani na vipindi vya jua.Mara tu yatokeapo mabadiliko ya hali ya hewa uathiri sana mfumo mzima wa ulajisamaki katika kula.Pia hali ya baridi sana na ikiwemo  mabadiliko ya ghafla katikahali ya hewa hupelekea ulaji wao kuwa mdogo na wakati mwingine kutokula kabisa.
2.      Kwa kawida samaki hawali vizuri katika hali ya misukosuko ambayo husababishwa na viumbe wala nyama,uvunaji wa mara kwa mara katika bwawa,kutokuwa na maji bora na salama n.k.Pia ongezeko la joto ambalo ni tatizo na pia upelekea upungufu wa hewa ya oxygen katika maji.
2.namna ya ulishaji samaki
Kawaida jamii ya samaki aina ya sato/pelege hula kwa kutupia chakula ndani ya bwawa lako.wakati mwingine kunakuwa na maeneo maalumu ya kulishia au kutengenezea maeneo mbadala ya kuwekea chakula.Umuhimu wa kutenga maeneo mbadala ya kulishia ni hupelekea mara tu uwekapo chakula samaki hutambuana mara moja na kuanza kula chakula hicho.Chakula hicho Pia katika bwawa dogo kuwe na sehemu moja ya kulishia isipokuwa katika mabwawa makubwa kuwe na sehemu nyingi za kulishia.
 
3.Mudamaalumu kwa ajili ya ulishaji wa samaki
Kama sheria zinavyoelekeza,ukuwaji wa samaki wanaofugwa  katika ufugaji cha kati(wastani) wanatakiwa kula angalau mara mbili kwa siku.Wakati muhimu wa ulishaji samaki ni asubuhi kati (2:00 am-4:00 am)ikitegemea na hali ya hewa na kuchomoza kwa jua na pia jioni (10:00 pm-12:00pm)ikitegemea na hali ya hewa na kuzama kwa jua.Kwa upande wa samaki wadogo wao hutakiwa kula mara kwa mara,lakini katika kiwango kidogo.


Kabla ya kufanya ulishaji wa samaki wako kuna vitu vya muhimu kuzingatia:
·         Itakulazimu kuchelewesha ulishaji wa samaki,Kama asubuhi itakuwa na machafuko mengi na pia jua halijachomoza.
·         Ikiwa hapata kuwa na dalili yeyote ya samaki kuonekana mara tu ulishapo chakula,itakulazimu kusimamisha zoezi la ulishaji na kuchunguza tatizo lililopo kwenye bwawa.
·         Kama utafanya shughuli mbalimbali mfano uvunaji samaki,n.k na kupelekea mvurugano wa maji,itakulazimu kutolisha kwa wakati huo na kusubiri wakati ujao.
·         Kutofanya shughuli za ulishaji kwenye siku ambayo umepandikiza samaki wapya bwawani na siku ambayo umefanya matibabu ya samaki wako.

4.Kiwango cha chakula katika ulishaji
Samaki anaweza kulisha chakula kutokana na uzito walionao au kiwango kilichopo.Kiwango cha chakula kinachohusiana na uzito wa samaki alionao.Samaki hupatiwa chakula kutokana na kiwango kilichowekwa ambacho ni 3%-5% ya uzito walionao kila siku.Kwa kutumia njia hii ya ulishaji unatakiwa kujua wastani wa ukubwa wa samaki wako.Hii inaweza kupatikana katika kuchukuwa  uwiano  baadhi ya samaki mfano kila baada ya wiki mbili.Kwa kufanya hivi, tunatosa nyavu katika bwawa na kuchukua samaki wachache (kama samaki 10) kwa haraka unachukuwa jumla ya uzito wao na unawarudisha katika maji. Utagawanya ile jumla ya namba ya samaki uliyoipata (10 samaki) utapata idadi ya uzito ya kila samaki, kwa mfano jumla ya uzito wa kila samaki ni gram 50 na kwenye bwawa lako wapo samaki 1000, utapata jumla ya uzito wa samaki wote itakuwa ni 50kg. Jumla ya uwiano wa samaki kila siku utakuwa kati ya 1.5kg- 2.5kg.

5.AINA MBALIMBALI YA VYAKULA VINAVTOTUMIKA katika ulishaji
Vyakula vya viwandani (Pellets)
Hii ni aina ya chakula ambayo hutengenezwa viwandani na kuuzwa katika masoko mbalimbali. Aina hii ya chakula(pellets) hupatikana katika muundo tofauti mfano vyakula vinavyoelea na vinavyozama,hutegemeana na aina ya samaki wanaofugwa. Jamii ya sato wenyewe hupendelea vyakula ambavyo huelea lakini kwa jamii aina ya kamba na kamba kochi na kambale wenyewe hula  vyakula ambavyo vinapatikana chini ya maji.Chakula hiki kwa kawaida hupatika katika ukubwa tofauti,itamlazimu mfugaji kujua ukubwa wa samaki alionao kabla ya kufanya manunuzi ya chakula. Kwa samaki wadogo itakuwa ni vigumu kwao kuweza kula chakula hiki kwa sababu hakiendani na ukubwa wa midomo yao. Endapo utatumia chakula hiki kuwalisha itakuwa ni upotevu na uchafuzi wa maji kwa sababu hawataweza kukila vizuri.
Vyakula vya unga (Mash feeds)
Huu ni mchanganyiko wa mimea mbalimbali yanayopatikana kwenye ardhi na yenye virutubisho tofautitofauti.Ikumbukwe kwamba, baadhi ya mimea mingine huwa katika hali ya kugandiana ambayo  hupelekea kutotenganishwa katika usafirishaji, uhifadhi na ulishaji. Virutubisho vya vyakula hivi havina tofauti na vile vya pellets. Lakini tofauti kubwa iliyopo ni kwamba havipitishwi kwenye mashine(pelletized).Mchanganyiko huo wa chakula (mashfeed) ni vya kipekee, na mara nyingi hutumiwa  na kupendelewa zaidi na samaki wadogo (fingerlings) ambao bado hawajawa na uwezo wa kula pellet kubwa.Ingawaje ni nzuri kwa samaki wakubwa,lakini tatizo hujitokeza pale unapolisha zenyewe husambaa eneo kubwa la bwawa na kuwafanya samaki kutumia nguvu kubwa ilikuweza pata chakula cha kujitosheleza.
 
Mchanganyiko wa virutubisho mbalimbali (Ingredient Mixtures) 
Kawaida hutengenezwa na mkulima au wajasiriamali wadogo wadogo.Tofauti kubwa iliyopo kati ya hiki chakula na mash feeds ni kwamba virutubisho hivi vinapitishwa kwenye machine ya kuchanganyia na kupakiwa sehemu maalum kwa ajili ya uuzaji katika maeneo mbalimbali.Ingawaje chakula hiki licha ya kuwa na gharama ndogo lakini kina tatizo kubwa endapo virutubisho hivyo kama havita shikana vizuri,mfano kujitenga tenga na vingine au kupatikana sehemu moja zaidi kuliko nyingine hupelekea samaki kutopata uwiano sawa na samaki wengine na kuadhiri sehemu ya ukuwaji katika bwawa lako.Kwa mfano ukiwa unalisha wakati kuna upepo,vile vyepesi husafirishwa na upepo kutoka sehemu moja kwenda nyingine navile vyenye hali ya uzito huenda moja kwa moja kwenye vilishio.Hii inaashiria kwamba samaki waliopo katika bwawa hawataweza kupata virutubisho sawa na wengine katika hilo bwawa.

Vyakula vya aina tofauti (Separate ingredients) 
Kutokana na kutokuwa na utengenezaji wa chakula cha samaki,baadhi ya wakulima hupendelea kulisha samaki wao aina mbalimbali ya vyakula vipatikanavyo masokoni.Baadhi ya vyakula hivyo ni kama vile unga wa samaki,soya bean,mbegu za pamba,unga wa ngano,pumba za mpunga,damu (brood cake),n.k.Ingawaje  vyakula hivi ni vizuri kwa samaki lakini mkulima anatakiwa kuwa makini na viwango vya vya kula katika ulishaji.Ulishaji mkubwa wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha protini ni gharama (pia ulishaji mwingi wa chakula upelekea uchafunzi wa maji),ikubukwe kwamba ulishaji mdogo wa vyakula vya protini hupelekea uvunaji wa samaki wenye uzito mdogo.
6.URUTUBISHAJI WA BWAWA
Umuhimu wa urutubishaji
·         Inaongeza ubora na wingi wa chakula cha asili kwa samaki.
·         Mbolea husaidia kuongeza rutuba kwenye udongo hasa katika mabwawa ya udongo.
·         Urutubishaji pia husaidia kuzuia maadui wa samaki kama vile ndege na baadhi ya wanyama wengine kwasababu maji yaliyo rutubishwa hayaruhusu kuona kilichopo ndani kwa urahisi.


7.AINA YA VIRUTUBISHO
Katika ufugaji wa wastani, urutubishaji wa bwawa hutumika kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa vyakula vya asili ndani ya maji. Mabaki ya vyakula hutumiwa kama chakula cha samaki kwa ajili ya kuongeza uzalishaji. Moja wapo tunaweza kutumia mbolea, (mfano. farmyard manure, compost manure, animal wastes,etc). Pia tunaweza kutumia mbolea ambazo hupatikana viwandani mfano CAN (Calcium Ammonium Nitrate)au urea ambayo tunaweka kwa kiasi cha 2g per meter square na DAP (Di-Ammonium Phosphate) kwa 3g per meter square.
Urutubishaji kwa kutumia mbolea za viwandani: kwa kawaida mbolea hii  huyeyushwa katika maji kabla ya kuiweka kwenye bwawa. Ikiwa kama hutofanya hivyo na kuiweka kwenye bwawa bila kuyeyushwa huenda mpaka kwenye kitako cha bwawa na  baadhi ya virutubisho kupotea  kwa sababu vitashindwa kuyeyuka.
 
8.NJIA ZA URUTUBISHAJI
Kuna njia mbalimbali zinazotumiwa kwa ajili ya kurutubisha bwawa
NJIA YA KWANZA
·         Kusambaza mbolea au kirutubishaji katika kitako cha bwawa lako kabla ya kuweka maji
·         Weka maji kwenye bwawa kiasi cha inchi 6, na kuacha ndani ya wiki mbili.
·         Kujaza maji katika bwawa kwa kiwango kinachohitajika pale maji yanapoanza kubadilika kuwa kijani.
NJIA YA PILI
·         Kutengeneza sehemu maalumu ya uwekaji wa mbolea katika kona moja ya bwawa kwa kutumia vijiti vilivyokaribiana


·         Weka mbolea  katika eneo lililotengenezwa kwa kuwekewa mbolea katika kona ya bwawa
·         Tunaruhusu maji yaingie kwenye bwawa kwa kiwango maalumu

NJIA YA TATU
·         Kujaza mbolea katika kiroba kilichotengenezwa kwa matundu madogo madogo.
·         Hakikisha unafunga kiroba vizuri kwa kamba imara kabla ya kuweka ndani ya maji.
·         Weka kitu chenye uzito sawa na mbolea kati bwawa na funga vizuri eneo moja la kiroba.
·         Hakikisha kiroba chako kina elea ndani ya maji bila kugusa kitako cha bwawa(overhang).
 
NJIA YA NNE
Hakikisha unapima vizuri mbolea ya kiwandani kwa vipimo vilivyoelezwa hapo juu,wingi au udogo wa utumiaji wa mbolea hii utategemeana na ukubwa wa bwawa.
 

Tumia chombo kuchukulia kiwango cha maji katika bwawa na changanya na mbolea iliyotayari pimwa na hakikisha yote imeyeyuka kabla ya matumizi.


Mimina maji yenye mchanganyiko na mbolea katika maji ya bwawa kuzunguka pembezoni mwa bwawa na hakikisha ukiendelea kuikoroga vizuri.

9.JINSI YA UVUNAJI SAMAKI KATIKA MABWAWA
Katika bwawa tunaweza kufanya uvunaji wa jumla(completely) au uvunaji kiasi fulani cha samaki unaowahitaji(partially).Uvunaji wa jumla wenyewe unahusisha uondoaji wa kila kitu ndani ya bwawa,huku uvunaji wa kiasi wenyewe hukihusisha uvunaji wa samaki kadhaa kama vile samaki wakubwa tu au kiwango fulani na kubaki wengine kwa ajili ya kuendelea na ukuwaji.

Kwa uvunaji wa kiasi,tunatosa nyavu katika bwawa na kuchukuwa ukubwa wa samaki unaohitaji au idadi ya samaki unayoihitaji kwa wakati huo.Wakati huo huo wale wengine watakaobaki huna budi kuwarejesha kwa haraka katika maji kwa kuendelea na ukuwaji.
Kwa upande mwingine,tunapofanya uvunaji wa jumla tunatosa nyavu katika bwawa zaidi ya mara mbili mpaka tatu kadiri iwezekanavyo.Mara baada ya kutosa nyavu tunaondoa maji katika bwawa na kukusanya wale samaki walio baki baada ya utosaji nyavu na kuwaweka katika chombo maalumu.Kwa hali ya kawaida wale samaki ambao uvunwa kwa kutumia nyavu wanakuwa katika hali ya usafi kuliko wale wanaookotwa mara  baada ya utoaji maji.MWISHO
*Kumbuka pamoja na kusoma muongozo huu wa ufugaji wa samaki nakuelewa,bado ushirikishwaji wa wataalamu katika kila hatua ni muhimu sana kwa ajili ya kupata mavuno mazuri zaidi.
*ukiwa kama umeguswa,na umependezewa na muongozo huu wa ufugaji wa samaki,ukiwa kama mzarendo wa kukuza na kuendeleza sekta ya uvuvi kupitia ufugaji wa samaki,unaweza kuchangia mchango wako katika blog hii kwa ajili ya kuzidi kuandaa machapisho mengi zaidi yatakayo kufanya wewe kufanya vizuri zaidi.Na pia kuboresha blog hii kupata habari mpya kila siku juu ya ufugaji wa samaki nchini na duniani.
*Changia kupitia nambari 0718 986 328 au 0686 479 348.
*Naamini usomaji wa maelezo haya ni zaidi ya kitabu ambacho ungeweza kukinunua kwa gharama zaidi madukani,hata hivyo ni vigumu pia kujua vinapatikanaje.
*mungu awabariki sana kwa moyo na imani ya kusoma muongozo huu.
AHSANTE

 


6 comments:

Mainda Chanyika said...

Ni makala yenye kuelimisha sana - Imetuzindua.

Mainda Chanyika said...

Ni ni kijarida chenye mafundisho mazuri na chenye kuhamasisha. Ni kitu kizuri chenye kuelimisha na tunatakiwa tubadilike ili kuokoa uharibifu wa mazingira. Ufugaji wa samaki utapelekea kupungua kwa uvuvi haramu.

Mainda Chanyika said...

Ni chapisho lenye kuelimisha sana na kuhamasisha ufugaji wa samaki. Ni kitu kizuri na kimetoa elimu ambayo itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na uvuvi haramu. Ni elimu ya ukombozi kutokana na umaskini uliokidhiri

Mainda Chanyika said...

Ni chapisho zuri lenye kuelimisha na ambalo litasaidia kuondoa sintofahamu zilizopo kuhusu ufugaji wa samaki. Elimu hii itasaidia sana katika kuokoa uharibifu wa mazingira unaotokana na uvuvi haramu unaofanyika ili kukidhi mahitaji ya samaki

samaki farm said...

AHSANTE SANA MCHANGO WAKO.

Paskazia said...

Asante kwa kujitolea kwenu kuelimisha watanzania wenzenu pasipo choyo.Hiyo elimu ni sawa na kumpeleka mtu kozi lakini mmeitoa bure.Mimi binafsi nimependezewa nayo na ninatarajia kufanya huu mradi wa samaki mara mipangilio itakapokuwa kuwa imekamilika zaidi.Nilikuwa nafikiria nitaanzaje hapo nimefarijika zaidi baada ya kona taarifa zenu.Tupo pamoja.Asanteni na Mungu aendelee kwapigania katika hii kazi mnayoifanya.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa