Wednesday, 16 July 2014

WAFUGAJI WA SAMAKI KUTOKA KUSINI WANENA KWAMBA BIASHARA YA SAMAKI NI NZURI KILIKO BIASHARA YA KULIMA CHUMVI.


Picha ikionesha bwana Musa said Afisa mradi (kutoka kushoto mwenye begi) kutoka shirika la umoja wa wafugaji samaki Mtwara akiwa na bwana Dastani kutoka shirika la ReCoMAP.Ziara hiyo iliyofanyika katika kijiji cha mbuo Mtwara kwa ajili ya kukagua miradi iliyoachwa na shirika hilo  mwaka 2011.Mandhali yakionesha maeneo ya miradi ya mashamba ya chumvi ambayo yalipelekea wakulima wa chumvi kuhamasika kuanza ufugaji wa samaki.

Mahojiano yakiendelea baina ya wafugaji wa samaki ambao ni wakulima wa chumvi ambao kwa ushuhuda wao wakilalamika kwamba katika biashara ya uzalishaji chumvi ni ngumu na haina maslai kwako ukilinganisha na faida za ufugaji wa samaki.


 picha ikionesha moja ya mabwawa ya samaki katika fukwe za mwambao wa bahari ya hindi mkoa wa Mtwara,ufugaji katika mabwawa hayo.samaki ambao hufugwa katika mabwawa hayo ni samaki wa maji chumvi aina ya mwatiko au milk fish kwa jina la kitaalamu.
mashine ya kutumia upepo ambayo kwa sasa imekufa lengo kuu ya mashine hiyo ni kusukuma maji kutoka baharini na kuingiza katika mabwawa ya samaki.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa