Thursday, 7 August 2014

JE HUWA TUNAZINGATIA HAYAMWONGOZO WA AWALI JINSI YA KUANDAA BWAWA LA SAMAKI KABLA YA UPANDIKIZAJI WA VIFARANGA VYA SAMAKI.


MUONGOZO HUU UMEANDALIWA AFISA MRADI UWASA
Musa S.Ngametwa
Mawasiliano;0718986328
Kwa swali ama ushauri kuhusu muongozo huu.

MAANDALIZI YA BWAWA LA SAMAKI  KABLA YA UPANDIKIZAJI WA VIFARANGA.

UTANGULIZI
Ufugaji wa samaki ni ya shughuli ya kiuchumi anayo mwezesha mwananchi kujikwamua kutoka katika hali ya umaskini,yote haya yanawezekana kwa kuzingatia hatua zote muhimu zinazofaa katika ufugaji wa samaki.
Wafugaji wengi hukutana na changamoto nyingi sana katika ufugaji wao wa samaki na hata kufikia hatua ya kukata tamaa kwa kuona kwamba mitaji na nguvu wanayo tumia ni mikubwa kuliko faida na kipato wanachokipata.
Wafugaji wengi wa samaki wanashindwa kupata mafanikio au mavuno mazuri kutokana na kukosa au kushindwa kuwa na elimu ya kutosha na ustadi juu ya kile wanachokifanya katika shughuli nzima ya ufugaji wa samaki kuanzia hatua ya awali mpaka wakati mavuno au hatua ya mwisho.
Kupitia mwongo huu uta msaidia mfugaji wa samaki kutambua na kufahamu mambo yapi muhimu aliyokuwa anakosea katika hatua za awali na nini afanye kukabiliana na changamoto katika maandalizi ya bwawa kabla ya upandikizaji.

BAADHI YA MAKOSA AU MAPUNGUFU YANAYO FANYWA NA WAFUGAJI WA SAMAKI YANAYOPELEKEA KUWA NA MAVUNO HAFIFU KWA KUTOZINGATIA HATUA MUHIMU ZA MAANDALIZI KATIKA BWAWA LA SAMAKI.
1:Maandalizi yasiyo rasmi katika bwawa la samaki;
Hili ni moja ya mapungufu au ni kosa kubwa katika shughuli ya ufugaji samaki ambao wafugaji wengi huyafanya,mfano Mzee Kuota ni mfugaji wa samaki wa samaki wa muda mrefu sana,lakini kawaida yake kila anapo maliza kuvuna samaki katika bwawa lake huyaacha yale maji ndani ya bwawa mpaka pale inapokaribia muda mwingine wa kupanda mbegu ndio hutoa maji na kuweka mengine na kuanza kupandikiza mbegu.
MADHARA YAKE.
Endapo maji uliyomaliza kuvulia samaki wako hukuyatoa kwa wakati ule uliomaliza kuvua,unapelekea kuendelea kuzaliana kwa wadudu wadogo wadogo hujulikana kama bakteria ambao ni hatarishi kwa samaki,madhara yake bakteria wanaweza kushambulia samaki au vifaranga vya samaki kupelekea kupata magonjwa kama vile fangasi,hivyo mfugaji huendelea kuhesabu kuwa nimepandikiza vifaranga 3000 na anaweka mategemeo ya kuvuna 3000 au 2800 pasi kujua kwamba vile vifaranga alivyopandikiza vilishakufa tangu wakiwa wadogo kwa kushambuliwa na wadudu,hivyo mfugaji hukuta mategemeo aliyoyategemea kuyapata ni tofauti,hali kama hiyo humsononesha mfugaji kwa kukata tamaa wa kuendelea na mradi pasi kujua kama alikosea wapi katika maandalizi ya awali katika bwawa

Vile vile husababisha kuoza kwa udongo hali inayopelekea harufu mbaya na endapo mkulima asipotoa ule udongo wa awali hupelekea ukuaji hafifu kwa samaki kutoka kushindwa kupata hewa safi wakati wote.

1
Picha za baadhi ya vijidudu ambavyo ni hatarishi kwa samaki (bacteria)

2:kutofanya matengenezo ya bwawa kwa uhakika;
 Baadhi ya matengenezo muhimu ni kama vile kuhakikisha kuwa kuta ziko imara,kutotoa udongo            wa chini,kutochimba au kuongeza kina cha bwa kufikia mita zisipungua moja.

3:kujaza maji kabla ya kuweka dawa ya kuuwa vijidudu katika bwawa;
Mara nyingi hushauriwa kuweka chokaa kitaalamu hujulikana kama hydrated lime,ambayo moja kwa moja huenda kuua vijidudu vidogo vidogo ambavyo ni hatarishi kwa samaki.

4:kutorutubisha bwawa  kwa kutumia  mbolea;
Mbolea ambayo ni nzuri zaidi ya kurutubishwa bwawa kama vile ya kuku,ng’ombe,au mabaki ya mifugo  mingine,kutofanya hivi unapelekea kuwa  kutokuwa na chakula cha ziada  kwa samaki pindi chakula  cha kutengenezwa  kutokuwepo na wafugaji wengi wa samaki baada ya mavuno hutoa maji na kujaza maji  mapya bila kuweka mbolea kwa ajili ya urutubishaji wa bwawa kusaidia  kuzalishwa chakula cha asili .

Hayo ni baadhi ya mapungufu ambayo wafugaji wengi wa samaki huyafanya pasi na kuyafahamu hali inayowapelekea kulalama na kwa kutopata faida kupitia  mradi wa ufugaji samaki.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA MAANDALIZI YA BWAWA LA SAMAKI
1.      Kuhakikisha yale maji uliyomalizia kuvuna samaki wako unayatoa yote lengo ni kuzuia kuendelea kuoza kwa udongo na kuzaliana  kwa vijidudu hatarishi kama backteria na fangasi ambavyo hupelekea madhala wakati wa upandikizaji wa mbegu mpya.
2.      Kufanyia bwawa matengenezo kwa kutoa udongo uliopo chini ya bwawa kuongeza kina cha bwawa kama kimepungua chini ya mita  moja endapo bwawa lipo chini ya mita  moja linapelekea hapo baadae wadudu kama vile ndege, mkuli (otter) na wezi kuiba kwa urahisi
kuongeza  upana wa tuta kuhakikisha uimara wa ukuta unakuwa wa uhakika dhidi ya wadudu watoboao ukuta na nguvu ya maji kutopasua ukuta.

3.      Uwekaji wa chokaa ijulikanayo kitaalamu kama Hydrated lime.

Picha zinazo onesha mtu akimwagia chokaa ndani bwawa na picha nyingine ni mfuko wa chokaa ujilika nao kama lime

Faida ya uwekaji chokaa katika bwawa

(a)    Kuua vijidudu vyote ambavyo ni hatari kwa samaki mara nyingi vidudu hivyo sio rahisi kuviona kwa macho
(b) Inaongeza ubora wa udongo, husaidia kuzalisha kwa chakula cha  Asili ndani ya bwawa
(c) Inasaidia kupunguza kwa kuongezeka kwa kiwango cha asidi katika maji na kufanya  hali ya chemicali kwenye  bwawa kuwa sawa au inayo hitajika.3
4.      Uwekaji mbolea katika bwawa hii, husaidia kuzalishwa kwa chakula cha asili ndani ya            bwawa la samaki hivyo hupelekea kuongezeka .

Picha inayo onesha shughuli ya uwekaji wa mbolea ndani ya bwawa4
5.      Jaza bwawa maji kwa urefu usiopungua mita moja.


Picha inayo onesha tuta la bwala kwenye hali ya mlalo na kina cha maji kwenye bwawa.


Picha inayo onesha samaki ndani ya bwawa lililojazwa maji kwa mita moja,husaidia samaki kukua vizuri na kujinga na wadudu au wanyama walao samaki kama vile mkuli na ndege.

 Baada ya kusoma muongozo huu wa hatua ya mwanzo katika maandalizi ya bwawa kabla ya upandikizaji wa mbegu.
Matumaini yangu makubwa muongozo huu utafanyiwa kazi na kuzingatia hatua zake muhimu lengo kuhakikisha tunapata mavuno makubwa na yenye tija kwa kila mfugaji wa samaki.

MWISHO
5

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa