Sunday, 3 August 2014

NANE NANE

Baadhi ya watu waliotembelea banda la wakala wa mafunzo ya elimu ya uvuvi (FETA)wamevutiwa sana na jinsi wanajibiidisha kudahili wanafunzi vema kuhakikisha kuwa wanapambana na uvuvi haramu pamoja kukuza sekta ya uvuvi katika nyanja mbali mbali ikiwemo ufugaji wa samaki ambao kwa sasa unashika kasi katika maeneo mbali mbalimbali nchini.chuo cha FETA ambacho kwa hapo awali kilitambulika kama chuo cha uvuvi kikiwa na matawi mawili mbegani bagomoyo pwani,na nyegezi mwanza lakini kwa sasa kina matawi zaidi kufikia matano.Lakini kuongezeka kwa vyuo hivyo ni kukuwa pia kwa sekta ya uvuvi nchini ambayo kwa miaka mingi ilikuwa haipewi nafasi kubwa kwa jamii kuwa shughuli za uvuvi ni muhimu kwao na maendeleo ya jamii.Katika maonesho hayo yanayofanyika kijiji cha ngongo wilaya ya lindi mkoani lindi.wananchi wamejifunza mengi sana kuhusu uvuvi hasa hasara za uvuvi haramu lakini walio wengi wamehamasika kufanya ufugaji wa samaki katika maeneo yao kwa faida ya kiuchumi kwao na taifa kwa ujumla.Taarifa hii imeandaliwa na
 MUSA SAIDI NGAMETWA MTAALAMU WA UFUGAJI SAMAKI MTWARA TANZANIA.0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa