Monday, 4 August 2014

TUKIFANIKIWA KUTATUA MATATIZO HAYA....

Bado kunachangamoto nyingi sana ambazo huwa zinajitokeza katika miradi ya samaki na hasa kwa wafugaji wetu hapa nchini,leo naomba niweke machache tu ambayo kwa namna moja ama nyingine ndio kama kikwazo cha kuto pata mavuno mazuri katika ufugaji.

1.ENDAPO MFUGAJI WA SAMAKI UTAACHA KUJIAMULIA MAAMUZI MWENYEWE BILA KUMSHIRIKISHA MTAALAMU UTAFANIKIWA SANA;Kwa muda mrefu sana wafugaji wa samaki ambao bado wamekuwa wakijiamulia maamuzi yao wenyewe bila kumshirikisha mtaalamu katika mradi wake,baadhi ya maamuzi hufanywa na wafugaji kupitia vijarida na miongozo mbalimbali inayo patikana katika mitandao ambayo kwa kusoma tu pekee yake basi imejitosheleza kwa kuanza kutekeleza yeye mwenywe,hahahahah hapa wacha nicheke kwanza hivi ndugu yangu kwanini mashuleni wameweka masomo ya NADHALIA NA VITENDO?.Wacha kucopy na ku paste ndugu yangu matokeo yake unaanza kuona mradi haufai kwa uzembe wako mwenyewe,umesoma katika mtandao tu akaamua kuona sasa kila kitu unaweza,bwawa unachimba wewe,samaki unapandikiza wewe,chakula unatengeneza wewe na huduma nyingine je katika hayo yote unahakika kuwa ni sahihi kutekeleza wewe mwenyewe bila kuwa na mtaalamu na kwanini kuna watu maalumu waliacha kusomea computer wakasomea samaki tu pekee yake?,je ulishawahi kujiuliza hili swali.Hebu badilika ndugu yangu kila mtu achukue nafasi yake kwenye taaluma yake ili tuhakikishe kuwa unafanya mradi ukijua una wekeza kiasi gani na utaingiza kiasi gani.Usihofie kumtafuta mtaalamu eti kwa kuhofia gharama,gharama ya mtaalamu ni ndogo sana kuliko hasara ambayo unaweza kuipata.
2.TEKELEZA MAAGIZO UNAYOPEWA NA MTAALAMU.
Hii nayo ni moja ya changamoto ambayo mwisho wake hupelekea matokeo mabaya katika mavuno,wafugaji wengi wamekuwa na imani hafifu sana juu ya kile wanacho agizwa kufanya na wataalamu wao,naomba sana tujenge imani na wataalamu tutekeleza maagizo kwanza alafu kama maagizo yake haya kuweza kuzaa matunda hapo sasa unaweza kumuuliza mtaalamu vipi mbona hali imekuwa hivi atakupa sababu mtaitua na mwisho wa mradi mtaanza kupata mafanikio yaliyo bora na mazuri.
3.MJALI NA KUMTHAMINI MTU UNAEMUACHIA KUSIMAMIA MRADI WAKO.
Wengi wanao anzisha miradi hii ni watu wenyewe viwango tofauti za kiuchumi wapo ambao wanaanzisha na kuwaachia watu wengine wasimamie mradi yao,walio wengi hawapendi kuwajali na kuwathamini wafanyakazi wao ambao huwaachia kusimamia mradi huo,matokeo kibarua huyo na yeye kutosimamia kwa uadilifu mradi huo mfano kama kurisha na kusafisha utakuta hafanyi vile inavyo paswa,pia wakati mwingine wasimamizi hawa hawapewi mafunzo maalumu ya ufugaji wa samaki na wao wakajua nini cha kufanya wakati anafanya shughuli hiyo ya kusimamia mradi,walio wengi utakuta wanasimamia tu mradi kwa kuwa kijana katoka kijijini hana kazi anaambiwa akae hapo awe analishia samaki,pasi kujua A wala Z katika ufugaji wa samaki.
NI HAYA MACHACHE TARATIBU TUTAENDELEA KUJIFUNZA ZAIDI MAKOSA AMBAYO MOJA KWA MOJA MFUGAJI HUWEZI KUYAONA.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa