Friday, 22 August 2014

UFUGAJI WA KAA (CRAB)

 Picha ikionesha wanachuo kutoka chuo cha wakala wa elimu ya uvuvi Tanzania (FETA).Wakiwa katika moja ya kazi za vitendo (practical),ujenzi wa visimba vya ufugaji wa kaa,ufugaji wa kaa ni moja ya shughuli za ufugaji ambao hufugwa zaidi maeneo ya pwani kwani samaki hao aina ya kaa hufugwa katika maji chumvi (baharini),lakini katika ufugaji huu hujengi bwawa ni vizimba kama unavyo viona wanachuo hao walivyo kijenga kwa ustadi mkubwa.Kwa kila kizimba kimoja hukaa kaa mmoja na hapo kaa hunenepeshwa kwa muda wa miezi mitatatu mpaka sita kwa ajili ya kutimiza uzito kuanzia gramu 500-1000 kwa ajili kuuzwa sokoni,samaki huyu hupendwa sana na wageni kutoka nje na ndio maana soko kuu la samaki ni katika mahoteli.

Picha ikionesha mtaalamu wa fani ya ufugaji samaki akikagua moja ya miradi inayofanywa na wafugaji hao wa kaa katika kanda ya kusini katika mkoa wa Mtwara Tanzania.
Hii ni picha ya kaa ambae hufugwa na katika vizimba hivyo,ni samaki mtamu sana ingawa watu walio nje ya pwani hawapendelei sana kwa jinsi alivyo lakini ni moja ya samaki mtamu na mwenye protini ya kutosha.

KWA MAWASILIANO JUU YA TAALUMA YA UFUGAJI WA KAA WASILIANA NAMI
KWA SIMU NAMBA 0718 98 63 28 AU E-MAIL musasaid65@gmail.com

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa