Friday, 22 August 2014

VIJANA WENZANGU UVUVI WA MITUMBWI MPAKA LINI?picha mbali mbali zikionesha shughuli za uvuvi kwa kutumia mitumbwi,ambao vijana wengi wanatumia kama njia moja wapo ya kujiingizia kipato chao cha kila siku,swali la kujiuliza uvuvi huu duni wa kuvua samaki mpaka lini?,hakuna njia nyingine ya kuwapata hao samaki ambayo ni salama zaidi,hapa sitaki kusema kwamba uvuvi wa mitumbwi haulipi hapana.Ila kwa hali ya sasa sio kama ile ya babu zetu,hali ya sasa imebadilika sana na hasa upatikanaji wa samaki katika mito ,bahari ,maziwa na mabwawa.Huwa tunaenda kuvua kwa kutumia muda mwingi bila kujua kama tutapata au hatupati,ni hali inayobaki ya kusema kila siku tunamwachia mungu,kauli hii mpaka lini,sikatai kwamba kila jambo ni kumwachia mungu kwa yeye ni muumba mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani na kujua riziki za waja wake kila siku mpaka atakapo penda kumchukua.Kulingana na mabadiliko ya kisayansi na kitkinolojia kuna haja kubwa sana sasa kubadilisha mfumo huu wa upatikanaji wa samaki tukawa kama wenzetu wa china,misri,philipino na nchi nyingine zilizo endelea kupitia samaki.Naamini,tunaamini tukiamua inawezekana.
JE NI MFUMO GANI AMBAO TUKIACHA KUVUA UTATUSAIDIA SANA KAMA VIJANA NA SI TUISHI MAISHA BORA ZAIDI.
NJIA HIYO SIO NYINGINE NI UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MABWAWA TU.


ufugaji wa samaki katika mabwawa ni njia safi na salama na ya muda mfupi kutajirika kama kijana leo hii mimi na wewe tukiamu,vyanzo vya maji tunavyo vya kutosha sana hapa nchini,ni mtaji kidogo sana ambao unahitaji kuanza shughuli hii ya ufugaji wa samaki,na ndani ya miezi sita ya mwanzo ni kuanza kuvua samaki wako,hivyo ukiwa na mabwawa mengi kila baada ya wiki au mwezi ni mtu wa kuvua samaki wako kwa bei nzuri na yenye tija.Kupitia ufugaji wa samaki utakuwa umeepukana na hadha nyingi sana ambazo hapo awali ulikuwa unakutana nazo,mfano upepo mkali,mawimbi makali na zoluba nyingi za majini.

hakika hii ni picha ya kijana aliweka kando shughuli za uvuvi na kujikita zaidi katika ufugaji wa samaki na kama unavyoweza kumuona,amenawili na anavua samaki wake muda wowote bila kubahatisha,anauhakika wa kipato kuendesha familia yake na kusaidia jamii katika lishe,ile kauli yangua na hata viongozi wengi wa kitaifa na kimataifa ukiamua inawezekana.
Picha hii itakupa picha kamili sasa kumbe ufugaji katika mabwawa inawezekana nasio mradi wa kubahatisha kama wengine wanavyo utafsiri,ni mzigo mkubwa sana wa samaki wakivuliwa kutoka katika bwawa,picha ni wa philipino,je sisi watanzania tunashindwa tumeumbiwa na kasoro gani kwa mungu?.
KIJANA MWENZANGU MIMI NA WEWE TUONESHE KWA VITENDO TUNAUWEZO WA KUACHANA NA UVUVI WA MITUMBWI  YA MAKASIA NA KUJIWEKEZA KATIKA UFUGAJI.
Naitwa MUSA SAIDI NGAMETWA KUWA HURU MUDA TUJADILIANE SOTE KWA NJIA YA SIMU AU E MAIL TUNAJENGAJE UCHUMI WA NCHI KWA KUPITIA UFUGAJI WA SAMAKI UKIACHANA NA UVUVI.
0718 98 63 28 
e-mail-musasaid65@gmail.com

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa