Thursday, 23 October 2014

Mvuvi maskini sehemu ya pili.alilalamika Majuto. Aliwaza sana mpaka ghalfa wazo lilimjia –
“nitaenda kumuomba mchawi anisaidie na kuniondolea shida zangu zote”, alisema Majuto. Pamoja na
kuwa alishasikia kwa wazee wa kijijini na pia kwa watu wengi kuwa mchawi huyo aliyekuwa akiishi
milimani sio mtu mzuri, Majuto hakufikiri mara mbili. “Hii ndio nafasi yangu kubwa ya kuweza
kubadilisha maisha yangu kabisa. Hao wanaosema kuwa hili sio jambo zuri hawapendi kuniona
nimefanikiwa”, alisema Majuto.
Hadithi Ya Mvuvi Masikini
Siku ikawadia na Majuto alifungasha virago vyake, aliiaga familia yake na kubeba zawadi ambazo alikuwa
amemtayarishia mchawi. Bila kugeuka aliondoka upesi na kuelekea juu milimani alipokuwa akiishi huyo
mchawi. Safari ilikuwa ni ndefu lakini Majuto alikuwa akitembea upesi sana. Alivuka mito, mabonde na
misitu minene ambamo walikuwa wakiishi wanyama wengi wakali. Baada ya kutembea kwa muda mrefu
Majuto alijikuta akipita kwenye uwanja mkubwa na kwa ghafla alitokea ndege mkubwa sana angani.
Alikuwa na rangi ya zambarau na njano na mkia mrefu wa kuvutia. Majuto alishtuka sana alivyomuona
huyo ndege kwa kuwa hakuwahi tena kuona ndege mkubwa hivyo aliyeruka angani. Alisimama  mdomo
wake ukiwa wazi kwa mshangao. Ndege huyo alitua chini ardhini na alizidi kumsogelea Majuto. Jasho
jembamba lilimtoka Majuto na hakujua cha kufanya na alibaki amesimama tu bila kusema neno lolote.
Ndege alisimama na kumuangalia Majuto machoni kisha akasema kwa sauti nzito, “Mtaka vyote hukosa
vyote”. Kisha ndege aligeuka na kuruka angani na kupotea juu ya mawingu.  Majuto hakuamini
alichokiona na kusikia na alijihisi anaota. Alijaribu kutafakari lakini alikosa jibu na akaamua aendelee na
safari yake ya kwenda kwa mchawi.
Baada ya kutembea kwa muda mrefu Majuto hatimaye alifika kwenye nyumba aliyoishi mchawi. Ilikuwa
ni nyumba kubwa nyeupe iliyovutia sana. Mawe meupe yaliyo ng’aa yalikuwa yamepangwa vizuri
kuelekea hadi mlangoni. Majuto alikuwa anauoga lakini alijikaza na akagonga mlango. ”Nani wewe?”,
alisikia sauti ikitoka ndani ya nyumba. ”Ni mimi Majuto mvuvi masikini. Nimekuja kuomba msaada
wako”. Mlango ulifunguliwa na hapo alikuwa amesimama mzee mmoja mfupi mwenye mvi nyingi.
Alionekana ni mtu wa kawaida tu tofauti kabisa na hadithi zote alizokuwa amezisikia Majuto huko kijijini
kwake. Majuto aliwaza kuwa labda amekosea nyumba na huyu sio yule mchawi ambaye watu walikuwa
wakimsema. Ikabidi Majuto amulize ”je, wewe ndio mchawi?”. ”Ha ha ha” alicheka mzee, ”ndivyo watu
wanapenda kuniita hivyo. Karibu sana ndani”.
Majtuo aliingia na kukaa chini kwenye mkeka. ”Ninaweza kukusaidiaje?” aliuliza mchawi. ”Nimefunga
safari kutoka mbali kuja huku ili niombe msaada wako”, alisema Majuto. ”Mimi ni mvuvi lakini
ninaogopa  sana maji na hivyo inanizuiya kuweza kwenda mbali na ngalawa yangu ili nikatege  ndoano
yangu na kukamata  samaki. Kila ninavyowaza jinsi ya kufanya nashindwa na ninabakia tu kando kando
mwa  ziwa ambapo samaki ni wachache na pia ni wadogo. Ninakuomba sana unisaidie kuondoa uwoga
wangu wa maji ili niweze kujifunza kuogelea na kupata uhodari wa kwenda mbali zaidi na ngalawa
yangu.” ”Lo, nimekuelewa”, alisema mchawi. ”Tatizo lako ni dogo sana. Subiri hapa nitakuletea dawa
itakayo kusaidia”. Mchawi aliamka na kwenda uwani. Baada ya muda si mrefu alirudi huku ameshika
chungu kidogo chenye  kilichofanana na maziwa. Alimpa Majuto kile chungu na kumwambia  anywe. 
ENDELEA KUFUATILIA HADITHI YA MVUVI MASKINI SEHEMU YA TATU,KUJUA KAMA KWELI JE MAJUTO ALIKUNYWA ALICHOAMBIWA AU LAH......

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa