Thursday, 22 January 2015

MATUMIZI YA WATER PUMP

 Water pump katika ufugaji wa samaki ina kazi gani katika ufgaji wa samaki?,je inaongeza gharama yeyote katika mradi?na kitu kipi kinarazimu mpaka nitumie water pump?.

HAYO NI MOJA YA MASWALI AMBAYO WALIOWENGI HUJIKUTA WANAINGIA KATIKA MATUMIZI YA WATER PUMP PASI WAKATI MWINGINE KUTOKUWA NA ULAZIMA WA KUFANYA HIVYO.

1.Water pump ina kazi kuu mbili katika ufugaji wa samaki.(1)kuingiza maji ndani ya bwawa(2) kutoa maji kwenye bwawa..
2.Matumizi ya water pump inachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza gharama za mradi kwani inatumia mafuta kiasi na gharama ya ununuzi ya water pump yenye na hasa kama mradi ni kubwa,Hivyo endapo mfugaji mdogo unatumia njia hii ni dhahili kabisa kutoweza kuona faida ya ufugaji wa samaki.

3.Kuna sababu kadhaa zinazopelekea mtu kuingia kwenye matumiz ya water pump yasiyo ya ulazima na hasa katika mfumo wa kutolea maji,mfano kujenga bwawa pasi kuzingatia kanuni za ujenzi wa bwawa na mifumo ya kutolea maji,Hivyo wakati wa utoaji wa maji ina kuwia vigumu kwa mfugaji kutoa maji kirahisi,hivyo ni vema kwa mfugaji unayetaka kufanya ufugaji wa sa samaki katika mfumo ulio rahisi ni vema kuwaona wataalamu kwa ushauri ambao utakusaidi ni jinsi gani unaweza kujenga bwawa bora ambalo halito kugahrimu katika njia mbalimbali ikiwemo hii moja wapo ya gharama ya matumizi ya water pump katika sehemu isiyo hitaji matumizi ya mashine hii.
kwa maelezo haya nafikiri unaweza kujifunza kitu kupitia mtandao huu.

 Moja ya miundo mbinu ya mabwawa ambayo mifumo yake ya utoaji na uingazi wa maji unatumia water pump,ni mfumo mzuri lakini kwa wafugaji wa kiwango cha kati na kikubwa.
Moja wa mfugaji wa samaki akiwasha mashine ya maji,tayari kabisa kwa ajili ya kujaza katika bwawa lake,.Swali la kujiuliza mimi na wewe je maji haya yanaonekana kuwa ni safi na salama kwa ufugaji wa samaki?.na kama sio safi na salama ni kipi kifanyike,na kwanini mfugaji huyu anafanya hivyo.Picha hiyo inatoa taswira kwa wafugaji wa samaki walio wengi ambao wanatumia njia hiyo ambayo siyo rafiki katika ufugaji wasamaki.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa