Tuesday, 3 February 2015

TAMBUA MAJI YASIYOTAKIWA NDANI YA BWAWA LAKO..


 Uwepo wa maji wa aina kama hii sio salama kabisa kwa kuendelea kufugia samaki.Rangi kama hiyo ni kiashilia kimojawapo cha kuwa maji yako hayapo kwenye uhalisia wake wakaida.Sasa utatambuaje maji yanayotakiwa ndani ya bwawa lako ili upate matokeo bora na mazuri katika mradi wako?


 Haya ndio maji yanayotakiwa yawepo ndani ya bwawa lako,uwepo wa maji yaliyo kwenye rangi ya ukijani wa wastani ni kiashilio tosha kabisa kuwa maji yako yamerutubishwa vema kwa ajili ya chakula cha zaida kwa samaki ambacho kitapelekea ukuaji mzuri wa samaki na kwa wakati husika.


Picha hizi ni moja za mifano ya bacteria ambao wanaweza kushambulia samaki wako pasi kutambua ndani ya bwawa lako,wataalamu tunashauri kuwa karibu na wataalamu kuweza kugundua vitu ambavyo vinaweza kukuletea athari endapo usipo vifanya kwa uangalifu ukijua kuwa ni hali ya kawaida,hali ambayo wafugaji wengi kimewakuta na kusababisha athari kubwa katika ufugaji wao na hata kufikia hatua ya kukata tamaa.TUJIFUNZE KULINGANA NA MAKOSA SIKU ZOTE.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa