Tuesday, 3 February 2015

UKAGUZI WA ENEO LA MRADI NI HATUA MUHIMU KULIKO KITU CHOCHOTE....


 Picha ikionesha wataalamu wakikagua eneo la mradi katika wilaya ya Mkuranga kijiji cha Sunguvuni,hatua hii ni muhimu sana kabla ya jambo lolote lile katika kuanza utekelezaji wa mradi wako.Kuna faida nyingi sana endapo eneo lako litafanyiwa ukaguzi yakinifu na kutathimini eneo lako linafaa au halifai?,na kama halifai nini kifanyikie,tambua sio kila eneo linafaa kwa mradi wa samaki,au kama linafaa kwa kiwango gani,na aina gani ya ufugaji inakufaa,na ujenzi wa bwawa lako lijengwe la aina ipi mfano kwa kujengea na tofali,plastiki au kujengea kwa udongo.Unapo puuza hatua hii kwa kutojua,kukwepa gharama za wataalamu,kuna hasara kubwa sana ambayo unaweza kuipata,mfano unaweza kujenga sehemu ambayo mradi wako hautokuwa endelevu na imara,unaweza kujenga aina ya bwawa ambalo halipaswi kujenga katika hilo ulilolipanga n.k.Katika hatua hii ndio itatoa tathimini ya gharama nzima ya mradi,bila hatua hii mtaalamu itakuwa vigumu kukupa tathimini ya gharama ya mradi wako.Shughuli ya mradi wa ufugaji wa samaki wengi hujikuta wakianza kuulizia gharama za mradi upoje,kwenye hali ya kawaida kwa mtaalamu yeyote ambaye anafanya kwa misingi bora ya PROJECT MANAGEMENT ni vigumu kutoa tathimini kama hatua ya ukaguzi wa eneo haijafanyika.Kwa ufupi shughuli za ufugaji wa samaki hauna gharama kubwa na hasa katika uendeshaji wa mradi pindi miundo mbinu inapokamilika.

 Mazingira ya eneo ambalo mradi unataka ufanyike,ardhi kama hii ambayo ardhi yake ni ya kichanga,hauwezi kutuamisha maji kirahisi hivyo lazima ifanyike mbinu mbadala ya ujenzi wa bwawa ili shughuli ya ufugaji samaki uweze kuendelea.
 Tanki la kuhifadhia maji yanayotoka kwenye kisima tayari kabisa kwa ajili ya kuanza kujaza katika mabwawa ya samaki.Hivyo eneo hili linaonesha upatikanaji wa maji hauna shida.
 Katika mradi wa ufugaji wa samaki pia matumizi ya maji ya bomba hayana shida katika mradi,kikubwa wataalamu wanashauri kabla ya kuanza kujaza katika bwawa lako kuhakikisha maji hayo yanapimwa vizuri kulinganisha na mahitaji ya viwango vinavyo hiyajika kwa ajili ya kufugia samaki.

Mradi usiwe mbali na msimamizi wa mradi kwa ajili ya kuangalia usalama,na pia kusimamia mradi kwa umakini wahali ya juu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa