Thursday, 26 March 2015

Hii ni hasara ujenzi usiofuata kanuni bora


kwa muonekano ni muonekano wa bwawa zuri sana,lakini ujenzi huu ni wa kukopi na kupesti?.Jamani tutafika kweli?.Bwawa hilo mtu siye mtaalamu aliona kwa jilani na yeye kuamua kujenga bila kuzingatia taratibu na tabia ya udongo upoje,bwawa liweje na likaeje,mfumo wa maji kuingia na kutoka pia ukaeje,hakika kwa hili bwawa unavyoliona halikuwa na sehemu ya kutolea maji,sasa samaki watavuliwaje?,Pia bwawa hilo linapitisha maji,sasa hizi ni baadhi tu za dosari katika bwawa hilo,ndugu mfugaji umegundua kosa la huyu tujifunze vizuri nasi tusirejee makosa,mtaalamu huwezi kumkwepa kwa kusema wataalamu wanagharama sana,haya hebu angalia hasara aliyoipata hapa huyu mtu,na angemuita mtaalamu ni kipi bora?.Baada ya mtaalamu kufika na kubaini makosa hakuwa na jinsi ya kumwambia avunje bwawa na kujenga upyaaaa bwawa lake ili liwe bora na la kisasa kabisa.
Tuwatumie wataalamu vizuri wenye ujuzi na uzoefu wa kazi.Tuache ubabaishaji katika miradi,tusije kusema miradi hailipi kumbe wewe ndio chanzo chatolipa.
Ni hayo yangu kwa siku ya leo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa