Wednesday, 25 March 2015

MAANDALIZI YA UJENZI WA BWAWA YAKIENDELEA...

Picha  zikionesha baadhi za hatua mbalimbali katika uchimbaji wa bwawa bora na la kisasa kabisa kwa bei nafuu,wataalamu pia baada na kumaliza kufanya kazi ya udadisi wa eneo na kujiridhisha vema,hatua ya pili ni kupima eneo kama baadhi ya picha zinavyo onekana.Wachimbaji wakitumia zana za mkono wakiwa kwenye makundi wakipanga namna gani kazi itafanyika katika kiwango kizuri bila kukosea.Hakika kazi ya ujenzi wa bwawa sio kazi rahisi kama wengi wanavyodhani,wafugaji wengi hudhani kazi hii ya ujenzi wa bwawa hata fundi nyumba pia anaweza kujenga bwawa,jambo ambalo sio sahihi na wengi wao mabwawa yao huishia kupasuka kabla ya msimu ya mavuno jambo ambalo humletea hasara kubwa na kuona kama shughuli haina maslai,jambo ambalo si la kweli.
Ndugu yangu ufugaji wa samaki ni biashara kama biashara nyingine inahitaji ujuzi na uwelewe vema sio kukurupuka,wataalamu wazalendo wapo kwa ajili ya kukufanya uone biashara hii inatija na faida kwako,watakupa ushauri na wa busara bila kujali kiwango cha maslai.Hakika huu ni wakati wakutumia fulsa hii pekee.Kwa maswali ama maoni wasiliana nasi kwa anuani zetu hapo juu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa