Friday, 27 March 2015

MTAALAMU AKIKEMEA BAADHI YA WAFUGAJI WASIOFUATA KANUNI NA TARATIBU ZA URUTUBISHWAJI BWAWA.

Picha ikionesha mtaalamu wa miradi akikisitiza jambo fulani kwa wafugaji wa samaki.Siku za karibuni tangu biashara hii ianze ya ufugaji wa samaki wafugaji wengi wamekuwa wakikurupuka na kufanya maamuzi yasiyo sahihi na yasiofuata kanuni bora za ufugaji.Hali hiyo ya wafugaji hujikuta wakitumia fedha nyingi katika uwekezaji wa miradi hii kwa kusoma tu taarifa kutoka katika mitandao na vitabu vya miongozo ya ufugaji,mtaalamu huyo alitolea ushuhuda wa tukio lililofanywa na mfugaji wa samaki (eneo tunalifadhi) akitumia sabuni ya OMO kuuwa wadudu na kusafisha bwawa la samaki kabla hajapandikiza vifaranga vya samaki.Sasa Watanzania wenzangu tujiulize hivi kweli hizo ndizo kanuni bora wanazotuelekeza wataalumu wetu?,katika mahojiano yalifanywa mtaalamu wa kampuni yetu ya AQUES ltd Tanzania bw Emmanuel Maneno dhidi ya mfugaji alibaini kwamba watu wengi hudhani usafisha bwawa na kurutubisha kwa njia isiyo rasmi,akitolea mfano wa mmoja wawafugaji aliyesafisha bwawa lake kwa kutumia sabuni ya OMO,jambo ambalo sio sahihi na hakuna kanuni kama hiyo katika ufugaji wa samaki,akieleza kwa masikitiko makubwa sana kwani baadhi ya wafugaji kama hao ndio huwa wa kwanza kutangaza kwamba samaki hakui vizuri na kuonesha biashara hii haina faida,lakini tujiulize biashara haina faida kwa Tanzania tu?,hali ya kuwa nchi za jirani kama Kenya na Uganda zikionesha kufanya vizuri zaidi kuliko sisi!!!........,Lakini kama kampuni inajitolea kwa dhati kabisa kusaidia watanzania kwa njia ya mtandao kutambua kitu sahihi cha kufanya ili kufikia mafanikio yako kama watu wengi,Kikubwa ni ushirikishwaji mzuri wa mtaalamu kabla ya kuanza mradi wako.Kama inavyoeleza kanuni za mafanikio katika mradi wowote ule unaotaka kuufanya:-
1:UTAFITI /UPEPELEZI.
2:MAONO YAKO WEWE,UNAONA NINI?
3:TAFUTA MAARIFA YA KUTOSHA.
4:UCHUNGUZI
5:KAACHINI WEKA MPANGO KAZI.
6:JINSI YA KUPATA MTAJI
7:ZINGATIA MIKATABA
8:WEKA BIDII KATIKA MRADI WAKO
9:ZINGATIA UBORA.
10:WEKA AKIBA.
Hizo ni baadhi tu za kanuni ambazo kama utazingatia vizuri unaweza sasa kufanikiwa vyema katika miradi yako,Bado bw Emmanuel Maneno anaendelea kusisitiza kwamba licha ya kufuata tu kanuni hizo bado anaendelea kwa kutaja taratibu au kanuni nyingine za mafanikio makubwa ambapo alitaja kama ifuatavyo:-
1:UGAWAJI WA MAJUKUMU KWA USAHIHI.(LEVERAGE)
2:USIMAMIZI WA HALI JUU.(CONTROL)
3:UBUNIFU KATIKA MRADI WAKO.(CREATIVITY)
4:KUPANUA MRADI WAKO.(EXPANSION)
5:KUONA MAFANIKIO (PREDACTABILITY).Hizo ni picha za sabuni ya unga aina ya OMO ambazo mfugaji mmoja wapo alitumia kwa ajili ya kusafisha bwawa,njia hiyo sio sahihi kabisa kusafishia bwawa.


 Picha za mifuko ya chokaa ambazo ndio njia pekee na bora katika urutubisha na usafishaji wa bwawa lako. 
Njia mbalimbali za namna kutumia chokaa kwa ajili ya kurutubisha bwawa lako,

 Mfano wa chokaa aliyofunguliwa.


KWA MAELEZO HAYO NDUGU WAFUGAJI NA MNAOTARAJIA KUANZA BIASHARA HII YA UFUGAJI WA SAMAKI MSIFANYE BIASHARA HII BILA KUSHIRIKISHA WATAALAMU,WASILIANA NASI KWA ANUANI ZETU HAPO JUU KWA MAELEZO ZAIDI.0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa