Wednesday, 13 May 2015

MBUNGE WA VITI MAALUMU MH:ANNA CHIKAWE AWAWEZESHA WAKINA MAMA ELFU MOJA KUJIFUNZA UFUGAJI SAMAKI MASASI MKOANI MTWARA

 
Mh:Anna Chikawe akiwa pamoja na mtaalamu wa masuala ya ufugaji samaki bw:Musa Ngametwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo hayo kukamilika.Mh huyo alitoa msaada huo kwa wakina mama hao mkoani mtwara wilaya ya masasi kuwawezesha wakina mama wapatao 1000 kupata mafunzo ya ufugaji wa samaki ili waweze kujiari na kuachana na maisha tegemezi kutoka kwa wanaume.Wakina mama hao baada ya mafunzo hayo walitoa shukrani zao za dhati kwa Mbunge huyo kwani ni kitu cha kwanza katika historia mkoani hapo wakina mama kupata mafunzo ya ufugaji samaki,ikiwa na mahudhulio makubwa zaidi.
Hakika hii ni heshima kubwa kwa kitu alicho kifanya Mbunge huyo Mh:Anna Chikawe na uwe mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine hapa nchini kuwasaidia wakina mama kielimu zaidi za ujasilia mali ili kuwakomboa wakina mama.

 ukumbi wa Emirates Hall ulipo mkoani mtwara wilaya ya masasi ambapo yalifanyika mafunzo hayo ya ufugaji wa samaki.
 picha ikionesha viongozi mbalimbali waliofika katika mafunzo akiwemo mkuu mpya wa wilaya ya masasi ambaye alifungua mafunzo hayo ya kina mama juu ya ufugaji wa samaki.
 mkuu wa wilaya ya masasi aliyesimama akizungumza jambo kabla ya mafunzo.

picha za kinamama walio pata mafunzo hayo.Kwa hakika kupita mafunzo hayo ya ufugaji wa samaki ulifadhiliwa na mbunge wa viti maalumu Mh:Anna Chikawe yatawawezesha wakinamama kuinuka kiuchumi kwa kuanza miradi hiyo ya ufugaji wa samaki.
PONGEZI ZA DHATI KWA MH ANNA CHIKAWE KWA MOYO WAKE MKUNJUFU KWA KUJITOLEA KUWASAIDIA WAKINA MAMA KUPATA TAALUMA HIYO YA UFUGAJI SAMAKI,PIA SHUKRANI ZIMFIKIE  MUWEZESHAJI WA MAFUNZO HAYO BW;MUSA SAIDI NGAMETWA KUTOKA KAMPUNI YA AQUES LTD TANZANIA.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa