Saturday, 30 May 2015

VIJANA WENZANGU TUNAJINASUA VIPI NA TATIZO LA AJIRA?.

Tanzania ni moja ya nchi yenye vijana wengi wa nguvu kazi,lakini wengi wao kati yao hawatumikii vema nafasi na walilonalo.Elimu ni moja ya kikwazo kimojawapo kikubwa kinachofanya vijana wengi hapa nchini kushindwa kuwa na uwezo wa kujiamini na kuamini mawazo yao kuwa ni sahihi katika kujitengenezea njia za kujipatia kipato,kwa mfano kati ya vijana wanajishughulisha na kuamini mawazo yao kuwa ni sahihi wameweza kufanikiwa,na kuweza kutengenza ajira kwa wengine.Uwezo wa kijiamini,kujitambua,kuthubutu ni mojawapo ya changamoto inayopelekea vijana wengi kujiajiri.Baadhi ya wana falsafa wanasema kwamba kama nchini watu wake wengi wana uwezo mdogo wakufikili ni tatizo la ukosefu wa ajira lazima lizidi kukuwa.Kauli hii inatafasiri kuwa wengi wanashindwa kufikiri zaidi katika kubuni miradi ambayo ingeweza kuajiri watu wengine kama ilivyo kama ilivyo nchi nyingine.
moja ya picha ikiwaonesha wakisikiliza mada ya ujasilia mali.Kulala kwa kijana huyo ni kinaonesha kiashilio gani.


Kijana huyo akiwa kwenye boti kwa ajili kujipatia kipato chake.Ni vena vijana kuwa wabunifu wa miradi ili kuepuka na vishawishi vyakufanya mambo sio faa katika jamii.Moja miradi ya ufugaji samaki ambayo ni moja ya shughuli ambayo inaweza kusaidia vijana kujiari bila kutegemea ajira.Kwa sasa vijana inatupasa kubalika ili tulete chachu kwa taifa kukua kiuchumi.Moja ya njia ambazo za nje wameweza kupata utajiri na kupanua biashara kupitia miradi ya samaki.
VIJANA TUNASHINDWA KUAMUA.AMKA SASA KIJANA MWENZANGU MUDA NDIO HUU.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa