Saturday, 4 July 2015

AQUES LTD & NA VYUO VYA UVUVI (FETA) KATIKA HARAKATI ZA KUWAKOMBOA WAFUGAJI SAMAKI NCHINI.

 Kampuni ya AQUES LTD ikiwa chini ya wataalamu walibobea katika sayansi hii ya ufugaji wa viumbe maji (ufugaji samaki),inafanya harakati kubwa sana katika kuhabarisha umma wa Tanzania kupitia mtandao ambao watu wengi hujifunza na kupata taarifa muda wowote hivyo kwa waliofanya miradi wakiwa chini ya usimamizi wa wataalamu kutoka kampuni ya AQUES LTD wameweza kufikia malengo tarajiwa.
AQUES LTD inapozungumzia harakati haisiti kusema AHSANTE SANA FETA.FETA ni wakala wa elimu ya uvuvi hapa nchini Tanzania zamani kwa bagamoyo kilitambulika kama MBEGANI.Ili maendeleo yaweze kuonekana vema lazima ushirikiano uwepo,eidha wa moja kwa moja unatambulika ama kwa njia ya kawaida ambao AQUES LTD inafanya,huenda hata taasisi hizi za uvuvi hazifahamu ushirikiano huo upoje.AQUES LTD huwa inafanya kazi sana kwa kushirikiana na wanafunzi waliohitimu ama bado hawaja hitimu katika kuwaonganisha na wafugaji wa samaki ili wajifunze kwa vitendo na katika mazingira halisi ambayo ndio wafugaji wengi hapa nchini walivyo,kwa sasa uwezo wa wahitimu wengi kukaa nyumbani kama ilivyo hapo awali imepungua sana kwani miradi mikubwa ambayo huanzishwa na AQUES LTD huwatumia wanafunzi hao waliotoka katika taasisi za uvuvi FETA kusimamia miradi hiyo kwa ajili ya kujipatia uzoefu na weredi wa kazi hali inayowafanya wapatapo ajira rasmi kufanya kazi kwa weredi na ubunifu wa hali ya juu,kama tunashuhudia ubunifu unaofanywa na wahitimu kutoka vyuo vya uvuvi katika fani ya ufugaji samaki.

Wanafunzi wakiwa katika moja ya mafunzo kwa vitendo kwenye maabara ya chuo hicho FETA BAGAMOYO.Hakika sasa tunarajia ufugaji wa samaki utazidi kuonekana kutokana na wataalamu wanao andaliwa vema kutoka katika vyuo hivyo,ni furaha kubwa sana kwa wafugaji samaki kwani FETA atakuwa msaada mkubwa sana kwa kudahili wanafunzi wenye ufanisi na kazi.

Kijana Devocatus akiwa ameshika moja ya kifaa kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika fani hii ya ufugaji samaki.Devocatus ambaye yupo mwaka wa pili NTA LEVEL 5 anaelezea jinsi anavyo ipenda fani hii na hujisikia fahari sna anapoitwa mtaalamu wa ufgaji samaki.

 Ni mazingira duni ukiangalia kwa macho lakini mwanafunzi huyo amekubali kuishi humo pasi kujali mazingira mazuri aliyotoka kwa ajili ya kujifunza na kusaidia wafugaji samaki kuhakikisha kuwa wanapata mafanikio tarajiwa.
Picha ikionesha bwawa la samaki MADALA MTONI MKURANGA MKOANI PWANI  ambapo kijana huyo akifanya kazi kwa kipindi ambacho yupo likizo,bwawa hilo ambalo pia linasimamiwa na AQUES LTD ikiwa mmempa nafasi mwanafunzi huyo kutoka FETA BAGAMOYO kujifunza fani yake vizuri,huu ni moja ya kuonesha harakati kati ya AQUES na FETA  katika harakati za ufugaji wa samaki hapa nchini.

Unaweza kushangaa nini kinaendelea hapo.Mazingira ambayo mwanafunzi huyo akiwa katika mafunzo yake alikutana na changamoto ya chakula cha samaki kutokuwepo kwa mfugaji huyo.Lakini kijana huyo alichukua hatua licha ya kutokuwa kwa umeme alishauri kununuliwa kwa mashine ambayo itakuwa inatoa chakula katika mfumo wa tambi (pellet form).Huu ni moja ya ubunifu katika kazi kwani moja ya changamoto kubwa kwa wafugaji ni chakula cha samaki.

 Vizimba vidogo vilivyobuniwa vizuri kwa ajili ya uzalishaji wa kambale na kukuzia vifaranga.
Mashine ya chakula isiyotumia umeme ambayo inaweza kutumika sehemu yeyote ambapo hakuna umeme.
Devocatus akiangalia kwa mataminio bwawa analolisimia kwa sasa akitamani siku moja aje kumiliki bwawa kama hilo iwe ni moja ya sehemu yake ya ajira bila kutegemea serikali kama ilivyo ndoto nyingi za vijana.

HAKIKA FETA NA AQUES LTD SASA MTAKUWA MARAFIKI WAZURI KATIKA FANI HII YA UFUGAJI SAMAKI KUHAKIKISHA WAFUGAJI SAMAKI WANANUFAIKA KWA USHIRIKIANO HUU.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa