Friday, 3 July 2015

JE UNAFAHAMU UFUGAJI SAMAKI NA KILIMO CHA MBOGA MBOGA VINAENDANA?.

Watu wengi ama wafugaji wengi wa samaki wamekuwa hawafahamu kuwa ufugaji wa samaki ni rafiki mkubwa sana wa kilimo.Unapo fanya shughuli ya ufugaji wa samaki kwa kiasi fulani itasaidia kupunguza matumizi ya mbolea uliyopaswa kuweka kwenye mmea wako.
Tambua kuwa unapofuga samaki huwa na rangi ya ukijani ama kwa lugha nyingine maji yanakuwa yamerutubishwa,hivyo maji yale yaliyo rutubishwa vizuri kutoka kwenye bwawa lako la kufugia samaki unachukua na kumwagilia kwenye bustani ya mazao yako kuzunguka bwawa lako,mfano katika picha yetu utaona mfugaji samaki aliye amua kufanya shughuli ya ufugaji samaki na kilimo cha mboga mboga ingawa kwa upande wake yeye ilipendelea kulima bamia kando kando ya bwawa lako.
Hivyo kipindi cha kusubili mavuno ya samaki kilimo cha mboga mboga kinamsaidia sana kujiingizia kipato na kulisha familia yake.Kikubwa zaidi hulima msimu wote wa mwaka kupitia maji anayo yatoa kutoka kwenye bwawa.
Hakika AQUES LTD inafanya kazi nzuri sana ya kushauri wafugaji samaki hapa nchini Tanzania wawe na miradi mbadala kuzunguka mabwawa yao ili iwaongeze tija kuliko ilivyokuwa hapo awali mtu humwaga yote bila kufanya kazi yeyote,jambo ambalo wataalamu wa kampuni ya AQUES LTD waliona ni upotevu wa maji wa maji usio na tija,hivyo hubuni njia ya kufanya ufugaji wa samaki na kilimo bora kisicho tumia mbolea yeyote zaidi ya maji yanayotoka kwenye bwawa.

picha ikionesha mboga aina ya bamia ikiwa imezunguka bwawa la samaki.

picha ikionesha jinsi maji kutoka kwenye bwawa la samaki linavyoweza kustawisha mmea vizuri bila kutumia mbolea yeyote ile.
AQUES LTD inafanya kazi hii ya ubunifu ya ufugaji samaki kuwa rafiki mkubwa wa kilimo kumbunguza kula mboga mboga zinazotumia mbolea za kikemikali.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa