Saturday, 4 July 2015

KUWA MAKINI UNAPO TAFUTA MBEGU ZA SAMAKI KATIKA MZINGIRA YA ASILI.

Kwa msimu ya hivi karibu kampuni ya AQUES LTD katika pitapita zake za kutembelea wakulima sehemu mbalimbali hapa nchini ilikuta baadhi ya watu waliojenga mabwawa wakitafuta mbegu kwenye madimbwi yalio kando kando ya mto na mengine yalioingia kwa maji ya mvua.
Hatukatai kufanya hivyo lakini je tunajuaje ubora wa hizo mbegu unazo zitafuta kwenye hilo dimbwi unalotoa mbegu unzotarajia kuzipandikiza kwenye bwawa lako?.Chakuangalia hapa je hizo mbegu haina magonjwa,inakuwa katika ukubwa gani,je ndio hiyo aina ya samaki tunaotaka wafugwe kwenye bwawa ili wakuwe katika muda husika kama wataalamu wanavyo shauri.
AQUES LTD inashauri tusichukulie biashara ya ufugaji wa samaki kirahi rahisi kiasi kama hiki cha kuokota tu mbegu kwenye madimbwi,hakika kuona faida ya moja moja itakuwa ni vigumu na ndio vitu vinavyonpelekea baadhi ya wafugaji kulaumu wataalamu kwa jinsi wanavyozungumzia mradi wa huu na faida zake.Wafugaji tujaribu kuwaona wataalamu husika katika kila hatua kwa ajili ya kutoa na kukupa ushauri unaofaa kwa ajili ya kukupatia tija katika biashara ya hii ya ufugaji wa samaki.

picha ikionesha vijana wadogo ambao maranyingi ndio wanatumiwa kuvua samaki hao kwenye madimbwi na kisha kupandikizwa kwenye mabwawa.


 kwa picha hizi unaona samaki hao wawili utajuaje ni yupi anafaa kupandikizwa kwenye bwawa?.mweusi au mweupe?naomba jibu lako hapo.

Baadhi ya samaki ambao wanapatika zaidi kwenye madimbwi,katika hali kama hii wakiwa wadogo ni vigumu kujua yupi anafaa kupandikizwa kufugwa kwenye mabwawa.
NDUGU YANGU MFUGAJI AU UNAYETARAJIA KUFUGA SAMAKI AQUES LTD inakushauri kufuata taratibu za maradi huu wa ufugaji wa samaki na sio kujiamulia kwa kusoma tu vipeperushi na mitandao.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa