Wednesday, 2 December 2015

KUMBE INAWEZEKANA KUFUGA SAMAKI NYUMBANI KWANGU?

 Duh ilikuwa kama vile masihara kuamini macho baada ya kutembelea sehemu fulani katika harakati zangu kikazi nilizo pewa na wakuu wangu,nilona bibi na bwawa wakichimba bwawa lao wenyewe bila kuhitaji msaada wa mtu mwingine.Hakika kitendo hiki kilinifanya kufedheheka na kujiulizamengi sana ,hivi kumbe watu wamehamasika kiasi hiki mpaka kufanya ufugaji huu majumbani?.Bila kusita nikasogea na kuanza kwa salamu kwa kuwa ni wahehe ni kaanza na KAMWENEEE...kisha  kujibiwa na muzungumzo yakaendelea hakika nilivutiwa na namna walivyokuwa wanajieleza na kunifanya nijione kama shujaa kwa kile tunachokitoa kwenye mitandao watu wanakifanyia kazi,ikabidi nami niwaongezee maarifa zaidi na kuwa ahidi nitakuwa nao pamoja nao bila malipo yeyote.Nikazidi kuwatia moyo na kuwaambia ninyi ni watu wa mfano katika nchi juu ya kupambana na upungufu wa kiteo cha samaki hapa nchini.
Nilitamani sana kuona kila mtu anabwawa lake kadogo nyumbani kwake kama vile ilivyo nchi za Thailand,Taiwan na Ufulipino.
 Mr Ally Mbwana akiwa katika harakati za ujenzi wa bwawa lake dogo kwa ajili ya kitoweo cha nyumbani.
 picha ya bwawa katika hatua za mwisho wa bwawa.
 picha inaonesha akiwa anasawazisha bwawa lake.
bwawa likiwa limekamilika na kuanza kujaza maji.
HOOoooh Hakika ni zoezi ambalo linawezekana mimi wewe na yule kufanya hivi nyumbani kwetu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa