Wednesday, 2 December 2015

WAFUGAJI WENGI SANA WANASUMBULIWA NA TATIZO LA CHAKULA

Wafugaji wengi sana wa samaki hapana nchini wamekuwa wakijitahidi sana kujenga mabwawa wenyewe kufanya kila kitu wenyewe kiukweli mengi yapo chini ya ubora,lakini tatizo kubwa zaidi kuliko yote wafugaji wengi wamekuwa wanakosea sana sana kwenye upande wachakula jambo linalopelekea ukuaji samaki wao kuwa hafifu na kutokuwa katika muda husika.
Nimeshuhudia mara nyingi wafuga wakitengeneza chakula wenyewe ambacho mara nyingi chakula hicho hakina ubora wowote utakao mfanya samaki aweze kukua vizuri.
AQUES LTD inatoa angalizo wa wafugaji kutofanya hivyo kwani ni kosa kubwa linalowafanya kuchukua muda mwingi sana katika kukuza samaki wao,AQUES LTD inashauri sana wafugaji kuwaona wataalamu katika kila hatua ila kuhakikisha samaki wanakuwa vuzuri na ubora unaokubalika katika soko.
Moja ya chakula cha samaki ambacho kwa macho tu kinaonekana hakina ubora,jamani ndugu wafugaji wenzangu kwa hali hii tutachelewa sana kufikia malengo yetu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa