Thursday, 21 January 2016

SAMAKI ALIYEPUUZWA SANA SASA AWA DILI SOKONI.

Samaki aliyedhalaulika sana sokoni na hata majumbani kwa kuliwa na hata kibiashara sasa awa Kama lulu sokoni.Samaki aina ya kambale ni moja ya samaki ambao kwa kipindi cha hapo nyuma walikuwa hawafugwi kwa wingi sana hususani hapa nchini,lakini mwitikio mzuri wa wafugaji wa samaki umekuwa kwa kila mtu anayetaka kufuga samaki huyu,hata ughari wa kifaranga kimoja ni shilingi 500 tofauti kabisa na samaki aina ya sato ambacho chenyewe huuzwa shilingi 200.Uthamani wa bei hiyo kulinga na sababu mbalimbali hususani za uzalishaji na kadhalika,lakini pia katika ukuaji wa samaki huyu ndio kitu ambacho kimewavutia wengi sana huchukua muda usio zidi miezi sita hufikia wastani wa uzito gram 500 na kuendelea,na bei yake sokoni pia ni nzuri sana.
Hapo awali samaki huyu kila mtu akimuona ni kama lidudu Fulani ambapo watu walikuwa hawapaswi kumuona au kusikia,wengi husema samaki mchafu,mla tope samaki nyoka n.k.Lakini hali imekuwa tofauti sana siku izi juu ya samaki huyu katika sifa zake,zimekuwa sifa nzuri sana za kuvutia na kushawishi wengine,lakini harakati za wataalamu katika kuhamasisha jamii juu ya kutambua uthamani wa samaki huyu ulikuwa mkubwa japo awali ilikuwa ni vigumu watu kuelewa nini wataalamu wanataka.
Karibu na wewe uwe mfugaji mpya wa kambale kama walivyowengine kwa sasa.
 Kijana seif sangondo akiwa ameshika samaki aina ya kambale akiwa na wastani wa uzito wa gramu 800 kwa muda wa miezi sita tangu kupandwa kwake.

picha samaki aina ya kambale waliotoka kuvuliwa kwenye bwawa.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa