Wednesday, 10 February 2016

TUJIFUNZE KUPITIA MAKOSA YA WENZETU ILI TUFANIKIWE.

Kwa siku za hivi karibu kumekuwa na wataalamu wengi sana ,ambao hawana taaluma sahihi kabisa na ufugaji samaki,watu wengi sana wamekuwa wakiangukia katika mikono ya watu hawa,wamewaingiza sana watu hasara na kukata tama kabisa na hata mwingine huchelea kusema kuwa "Sitaki kabisa kusikia kuhusu samaki",hakika kauli hizi sio njema na zenye maumivu makali sana kwa anaye tamka.
Lakini tunajifunza nini kwa watu hawa?,umakini ni jambo zuri sana na kabla ya kufanya jambo lolote lile hakikisha umejifunza kwa kusoma na kutembea kuona watu wengine wamefanikiwa kiasi gani na huo mradi.
Hebu tujifunze kwa picha nini kilichokosewa nasi tujifunze.
 Picha ikionesha mtaalamu bwana Emmanuel maneno akimuhoji maswali mfugaji wa samaki.
 Moja ya bwawa la samaki lililojengwa ndani ya green house baada ya kushindwa kuzalisha.
makosa yaliyo katika bwawa hilo ni mfumo wa utoaji haupo jambo ambalo litagharimu katika utoaji wa maji kwa siku atakazo hitaji kuvuna samaki.
 Mmmh hapo sasa ,kwa elimu tunayo itoa je hivi kweli hayo maji ni sahihi?kwa hilo bwawa pia halina mfumo wa kutoa maji,naomba tusaidiane wote katika kuangalia dosari katika hilo bwawa ili na wewe kama bwawa lako lipo kama hilo toa taarifa mapema.
Muonekano kamili wa bwawa lililo ndani ya green hause ilyokufa.
Jifunze kitu kuhusu hizi picha.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa