Thursday, 4 February 2016

WATAALAMU WA AQUES LTD WAKITOA SOMO KWA WAFUGAJI SAMAKI WADOGO NCHINI.

Washiriki kutoka katika kampuni ya NAMAINGO iliyopo Ukonga Dar es salaam wakisikiliza kwa makini mafunzo ya ufugaji samaki kutoka kwa watalaamu wa ufugaji wa samaki nchini,semina hiyo iliojumuisha watu mbalimbali lakini mwitikio mkubwa sana waliojitokeza ni wakina mama ambao walikuwa kwa wingi zaidi,mafunzo yalitoa utambulisho kwa kutambua namna kampuni ya Aques ltd inavyofanya kazi na jamii.
Katika semina hiyo watu walipata fulsa ya kuuliza maswali mbalimbali juu ya ufugaji wa samaki hususani namna ya ujenzi wa bwawa la samaki,ujazaji wa maji,utoaji wa maji chakula cha samaki na upatikanaji wa mbegu za samaki husika mtu anaotaka kuwafuga.
 washikiriki wakifuatilia kwa makina mafunzo mafupi ya ufugaji samaki yaliyo endeshwa na kampuni ya AQUES LTD.
Mtaalamu Musa S.Ngametwa Akitoa maelekezo ya utambulisho wa awali kabla ya kumkaribisha Mr Emmanuel Maneno managing director wa kampuni ya Aques ltd kwa kueleza kwa kirefu zaidi.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa