Thursday, 14 April 2016

BADO MATUMIZI YA VIFAA VYA KISASA VINAHITAJIKA SANA KUDHIBITI UVUVI HARAMU HAPA NCHINI.

 Moja ya changamoto kubwa sana inazo zikabili sekta za uvuvi ni kukithiri kwa uvuvi haramu,jambo ambalo huharibu mazingira ya bahari na kufanya viumbe kutoweka,serikali imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kimaendeleo kuhakikisha kwamba tatizo hili linakwisha kabisa au kupongea.
Lakini kwanini jamii indelee kufanya uvuvi haramu kila uchwao wakati elimu ya matokeo hasi ya aina ya uvuvi huo haramu?bado kuna maswali mengi sana ya kujiuliza vipi kuhusu hukumu za watu wanapotia hatiani na aina ya adhabu wanazopewa je zinakidhi haja kulinga mapana ya kosa tunalo lijadiri,lakini mwisho kabisa serikali yetu ina dhana madhubuti ya kupambana na uvuvi haramu ikiwemo kufanya doria katika bahari kuu?.
Bado iko haja sasa watanzania tubadili mitazamo yetu na aina za uvuvi ,hapa sasa ndipo suala la ufugaji wa samaki napo linapata nafasi yake,hivi kama wewe unafuga samaki wako baada ya muda fulani umevuna na kuuza hivi umeepuka misuko suko mingapi katika bahari ziwani au mtoni.
Watanzani tupende kutii sharia bila kushurutishwa haswa katika matumizi ya nguvu.Hapa sitaki niwe mtoa somo katika suala Zima la uvuvi haramu hususani kutumia mabomu na kokolo.
Serikali pia iongeze na kutumia vifaa na dhana zakazi walizo nazo na kuziongeza pale zinapohitaji mfano matumizi ya ndege na helikopta katika kufanya doria wakati wote au nyakati maalumu kwa kushtukiza na pindi wanapowakamata kuwapa adhabu kali ili iwefundisho kwa wengine,pia kupitia upya sharia zake pale zinapolegalega katika adhabu na faini kulingana na aina ya kosa.

 picha ikonesha watu wakivua samaki kandokando mwa ziwa jambo ambalo hufanya upotevu wa samaki na uharibifu wa mazingira.
 wachuuzi wadogo wadogo wa samki wakinunua samaki hao wadogo waliovuliwa kwa njia haramu na kwenda kuwa uza kwenye masoko yao.
Baadhi ya wavuvi wakiwa wamekaa juu mtumbwi wakitafakari juu ya hatima yao endapo upatikanaji wa samaki hautokuwa wa karibu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa