Thursday, 14 April 2016

HONGERA WAZIRI WETU MWIGULU NCHEMBA KWA KAZI NZURI YA KUWATUMIKIA WATANZANIA.


Hongera sana Mh Waziri Mwigulu  nchemba kwa kazi yako nzuri unayo ifanya usiku na mchana,hapa sitozungumzia zaidi katika sekta au idara nyingine,hapa kwangu nasemea kwa upande wa  sekta uvuvi.
Itambulike kwamba ni kweli sekta ya uvuvi kwa kweli ni kama sehemu au ni sawa na familia iliyokosa wazazi japo kuwa wapo,imekosa malezi bora ,kila siku watu mbalimbali na baadhi ya viongozi husema kuwa uvuvi unalipa!uvuvi pekee yake unaweza kuinua nchi kiuchumi,lakini katika uhalisia wa kauli zao miaka yote haiukuwa na kitu.
Sekta hii ya uvuvi kwa miaka ya nyuma kuanzia miaka ya 2005 kushika chini sekta haikupewa kipaumbele sana katika kuonesha namna gani sekta hii imekuwa na tija kwa taifa,jambo ambalo lililopelekea hata sisi tuliosomea uvuvi unaona aibu kujitambulisha mbele ya wenzako kuwa unasomea uvuvi.
Sekta hii ikaja ikapa mtu sahihi kwa asilimia 100 kila mtanzania sikio lake likawa linajua mpaka idadi ya samaki na vifaranga vyake vilivyopo nchini,hali iliyopelekea hata idadi ya wahitimu katika sekta ya uvuvi kuongezeka na ajira kwa wahitimu hao kupatikana mara moja pindi wanapo hitimu.Hakika mh wetu waziri wa kipindi hicho JOHN P MAGUFULI aliitendea haki wizara hii,.
Mwenendo na harakati zako mh waziri unatupa imani mpya na kuanza kuhisi sasa tunaanza kurudi upya baada ya kupotea kwa muda mrefu,hakika unafanya kazi kubwa sana sisi kama wadau wakubwa katika sekta uvuvi hususani katika ufugaji wa samaki tunastahili kukupongeza kwa juhudi unazo zifanya za kuwatumikia watanzani kama alivyofanya na anavyofanya mh raisi J P M katika kuhakikisha watanzania wachini na sisi tunabadili maisha yetu kwa kiaisi Fulani.
Kwa juhudi za kazi zako mh waziri ukumbuke sana sekta hii ya uvuvi hususani kuipa kipaumbele sana ufugaji wa samaki hapa na kuhakikisha ajira rasmi kwa watu waliosemea masuala ya ufugaji samaki (Aquaculture),wape nafasi ya kuonekana wale wanao onesha juhudi za dhati kabisa katika kutoa hamasa juu ya ufugaji wa samaki ili mtu au kikundi kujiongezea kipato na kuongeza pato la taifa.
Katika safu tunakupoingeza sana na mungu akulinde kwani kwenye ukombozi kwa wanyonge vikwazo havikosekani,hakika mungu atakulinda na kukupa ujasiri zaidi.
 Picha ikimuonesha mh waziri akifanya kazi nyakati za usiku jambo ambalo ni vigumu kufanyika kwa viongozi walio wengi.
 Mh waziri akionesha ishara ya jambo fulani katika bwawa la samaki .
 

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa