Thursday, 14 April 2016

UFUGAJI WA KAMBALE KWA SASA UNASHIKA KASI HAPA NCHINI.

Katika hali isiyo yakawaida na isiyotegemewa na wafugaji wengi wa samaki hapa nchini na hata nathubutu kusema kuwa duniani kote kuwa ufugaji wa samaki aina ya kambale unaweza kukua kwa kasi kuliko ufugaji wa sato hivi sasa.
Wafugaji wengi sana walikuwa wanasita kufuga samaki aina ya kambale kwa sababu mbalimbali ikiwemo masuala mazima ya masoko,mazingira machafu ya kuishi kwa samaki huyu yaani kwenye matope hivyo wengi walikuwa hawapendeli hiyo hali na mwisho kabisa muonekano wa samaki huyu wengi wao walikuwa wanamuogopa kwa jinsi anavyo onekana.
Lakini sasa habari imekuwa tofauti kabisa na ilivyotarajiwa kwani wafugaji wengi wameweza kuelewa vizuri somo la ufugaji wa samaki aina ya kambale na kufuta fikra mbaya ambazo walikuwa nazo hapo awali,lakini hii haimaaminishi kuwa watu wasifuge Sato hapana.
Ukuaji wa samaki umekuwa ukiwafurahisha wafugaji sana na hivyo kuhamsisha na wengine ambao walikuwa wanaogopa kuingia biashara hii kwa hofu kuwa ukuaji hafifu wa samaki.
Hivyo watanzania bado tuna wasihi muendele kupitia ukurasa huu ili na sisi ifike wakati tuwe wafugaji wakubwa wa samaki kwa afrika na hatimaye dunia nzima.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa