Saturday, 16 April 2016

WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI MH MWIGULU NCHEMBA AKUTANA NA BALOZI WA IRELAND NCHINI.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Chemba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi. Fionnuala Gilsenan ofisini kwake katika jitihada zake za kuinua sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Waziri Nchemba alimweleza Balozi huyo kuhusu hali ya sekta ya kilimo na mikakati ya serikali katika kukabiliana na changamoto zinazokikumba kilimo chetu hapa nchini ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa mbegu, ambapo vituo vya utafiti vya serikali na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) vimejikita katika kutafiti mbegu mbali mbali.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa