Saturday, 14 May 2016

AQUES LTD KUTEMBELEA GAZETI LA MWANANCHI.

 Aques ltd katika juhudi zake za kuhakikisha kuwa jamii inazidi kupata taarifa ya miradi mbali mbali hapa nchini,safari hii iliona bora ikatembelee gazeti la Mwananchi makao makuu yake yaliyopo Tabata mkoani Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo moja ya jambo kuu amabalo wananchi watazidi kunufaika hususani kwa wale wasioweza kabisa kutumia mitandao kupata taarifa hizo kupitia kwenye gazeti wataweza kupata taarifa na maada zitakazo kuwa zinahusu ufugaji wa samaki tu pekee yake.
Hivyo Aques ltd inajitahidi kutekeleza malengo yake ya kuwa pamoja na wananchi kuhakikisha kuwa taifa letu la Tanzanzania linasonga mbele kupitia miradi mbalimbali hususani miradi ya samaki ambapo unaweza kufanya shughuli nyingine za kilimo.
 Wataalamu wa ufugaji samaki waliovalia vitambulisho vyenye rangi nyukundu wakimsikiliza mhariri wa gazeti la mwananchi walipotembelea ofisini kwao
 Mhariri wa gazeti la mwananchi akionesha namna ya upangiliaji wa habari unavyokuwa.
 Hiyo ni sehemu maalum kwa ajili ya kuandaa ukurasa wa gazeti uweze kuwa wa mvuto kwa wasomaji.
Mhariri wa gazeti la mwananchi akiwaonesha wataalamu wa ufugaji wa samaki Mr Musa s.Ngametwa aliyevalia fulana ya bluu na mr Emanuel Godfrey.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa