Saturday, 14 May 2016

AQUES LTD TANZANIA NA SON FISH FARMING COMPANY YA UGANDA SASA KUFANYA KAZI PAMOJA.

 Mtaalamu na Director wa AQUES LTD TANZANIA Mr Emmanuel Godfrey akiwa ameshika moja ya plastiki begi ni mfuko maalum kwa ajili ya usafirishaji wa samaki aina ya sato kutoka nchini Uganda tayari kwa safari ya kuja nchini,hatua hii ni moja ya kazi zinazofanywa na Aques ltd kuhakikisha kuwa Tanzania tunakuwa na mbegu bora kabisa hasa za samaki aina ya sato ambayo wafugaji wengi wamekuwa wakilalamika hazikui vizuri.Aques ltd wakishirikiana na kampuni mbalimbali za ndani na nje ya nchi kuhakikisha kuwa tunapata mbegu zilizo bora na kukua vizuri ili kila mfugaji apate tija katika biashara hii.
 Mifuko ikiwa imepakiwa vizurin kabisa kwa ajiri ya usafirishaji.
 Mr Emmanuel Godfrey akiwa tayari kusafirisha mbegu hizo kwa njia ya ndege kutokea jiji la Entebbe nchini Uganda kuja Tanzania.
Rubani wa ndege hiyo maalum iliyokdiwa kwa ajili ya kusafirsha samaki hao.
Hakika hizi ni moja ya juhudi kubwa sana ambazo watanzania kwa pamoja tunapaswa kuungana ili taifa letu linasonga mbele kupitia miradi hii ya ufugaji wa samaki.

1 comments:

mgalula Lyobah said...

Mwanzo Mzuri Katika Kukabiliana Na Changamoto Ya Mbegu Bora!!

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa