Saturday, 28 May 2016

FAHAMU HISTORIA YA UFUGAJI WA SAMAKI HAPA NCHINI KWA UFUPI.


Historia ya ufugaji wa samaki Tanzania haujawekwa vizuri kwenye maandishi, lakini kulingana na Balarin (1985) anasema majaribio yalianza mnamo mwaka 1949 katika mikoa ya Tanga (Korogwe) na Mwanza (Maly) ikionyesha kujengwa pia kwa mabwawa mengi ya samaki. Lakini mabwawa haya yaliishia kutofanya kazi kwasababu ya kukosa usimamiaji mzuri, matumizi ya technolojia isiyosahihi pamoja na matatizo mengine kama ya ukame na miundo mbinu mibovu. Kulingana na ripoti iliyotolewa na FAO mwaka 1968 ilionyesha kuwa Tanzania ilikuwa na mabwawa 8 000 ya kufugia samaki japo mengine yalikuwa madogo yenye uzalishaji kidogo.

Mwaka 1967 serikali ya Tanzania ilianzisha kampeni ya kuhamasisha ufugaji lakini haikuonesha mabadiliko makubwa. Mwaka 1972 kwa mara ya kwanza ufugaji wa samaki ulipewa umuhimu kisera japo sharia ilitungwa mwaka 1970. Mwaka 1997 sera ya ufugaji wa samaki ilipitishwa iliyoipa kipaombele ufugaji wa samaki.Ambapo chuo maendeleo ya uvuvi mbegani kilichopo bagamoyo kilikuwa kikitoa masomo hayo kwa ngazi ya cheti na diploma.Mwaka 2010-2011 kwa mara ya kwanza mafunzo ya ufugaji/ukuzaji viumbe maji vilianza rasmi (AQUACULTURE) kwa ngazi ya cheti na diploma ikiwa ni juhudi za serikali inazalisha wataalamu watakao husika na masuala ya ufugajji wa samaki tu pekee yake,na katika juhudi hizo serikali imefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana katika ukuzaji wa sekta hii .Lakini katika ngazi mbalimbali za elimu ya juu katika chuo cha kilimo SUA NA UDSM kutoa wataalam wa masuala ya ufugaji wa samaki/ukuzaji viumbe kwenye maji.

AQUES LTD NI MOJA YA KAMPUNI BORA TANZANIA INAYOENDESHWA NA WATAALAMU WALIOSOMEA TAALUMA HIYO YA UKUZAJI WA VIUMBE KWENYE HIVYO KUFANYA KWA UBORA NA UFANISI ZAIDI KATIKA MAJUKUMU YAO KIKAMILIFU NA WEREDI WA HALI YA JUU.

 

Pia matumizi ya samaki na hasa mafuta ya samaki ambayo ndo yanatumika sana kuwanywesha watoto wadogo yamethibitika kisayansi kuwa yanasaidia sana ukuaji wa ubongo wa mwanadamu. Lakini pia uwepo wa kiwango kidogo sana cha kolestero ambayo imeripotiwa kusababisha ugonjwa wa moyo kimepelekea ongezeko la watu wanakula samaki.

 

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa