Saturday, 28 May 2016

FAHAMU MIFUMO /NJIA ZA KUFUGA SAMAKI


Kuna aina tatu za ufugaji wa samaki:
1.       Ufugaji huria (extensive Culture system)

a)      Huu ni mfumo ambao samaki hupandikizwa kwenye bwawa na kuhudumiwa kwa kiwango kidogo  duni.

b)      Samaki hula vyakula vya asili vinavyo patikana kwenye bwawa.

c)       Samaki hupandikizwa wachache mfano mita 1 ya mraba inapandwa idadi ya samaki chini ya 3 na hivyo mavuno huwa kidogo.

d)      Mfumo huu maranyingi hutumika kwa matumizi  ya nyumbani tu kama mboga.

e)      Usimamizi wa aina ya bwawa hili huwa hafifu 

2.       Ufugaji nusu shadidi (semi-intensive culture system)

a)      Katika mfumo huu samaki hupandikizwa kwenye bwawa na kuhudumiwa kwa kiwango cha kati.

b)      Samaki hutegemea chakula cha asili na pia chakula cha ziada huongezwa katika bwawa. Mfumo huu ni mzuri na unataumiwa na nchi nyingi za Afrika.

c)       Mita moja  ya mraba tunapanda kati ya samaki 5-10

Mfano: kama eneo ni la bwawa ni chini ya mita za mraba 800m2 inashauriwa upande samaki 7 na kama bwawa lako ni zaidi ya mita za mraba 8002 unaweza kupanda samaki 10 na waka fanikiwa kukua vizuri, kwa uzoefu tumeona  samaki wanao kuwa katika eneo kubwa hukua zaidi kulikowanaokuwa katika eneo dogo.


 

     3.       Mfumo shadidi  (Intensive culture system).
a)      Huu ni mfumo unao tumia technolojia na utaalam wa kisasa kwani idadi ya samaki wanao pandwa katika eneo husika ni kubwa

b)      Samaki hutegemea chakula cha kusindika (Artificial feeds)

c)       Ufugaji huu unafaida na unahitaji mtaji mkubwa pia teknolojia ya  hali ya juu sana,ikiwa sambamba na miundombinu ya uhakika.

 

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa