Tuesday, 31 May 2016

FAIDA YA MIKOKO NA VIUMBE VINGINE KWENYE MAJI.

Mikoko ni miongoni mwa miti adimu ambayo inahifadhiwa na serikali kisheria kutokana na umuhimu wake kwa bayoanuwai katika ukanda wa pwani. Umuhimu wake ni pamoja na kuwa mazalia mazuri ya samaki, kuzuia chembe chembe za michanga zifike baharini na kuyafunika matumbawe na pia katika kuhifadhi mazingira ya pwani kwani huzuia mmomonyoko wa ukingo wa bahari na maingilio ya mito unaotokana na mawimbi makubwa ya bahari.

Mikoko hutumika kama makazi, chakula na mazalia ya samaki wakubwa, kamba wadogo na chaza
 Mikoko pia inawindwa kwa udi na uvumba na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kutokana na faida yake kubwa wanayoipata kwa kuuza miti hiyo. Mbali na matumizi mengine, miti ya mikoko hutumika kwa kutengenezea mashua. Pia hutumika kwa mkaa, ujenzi wa nyumba, dawa za miti shamba, uzalishaji wa asali na chakula cha mifugo kwa jamii mbalimbali za pwani na Zanzibar. Ni kutokana na faida hiyo, mikoko inazidi kukatwa hata kama ni kinyume cha sheria kukata miti hiyo. 

Serikali inatambua umuhimu wa mikoko na mustakabali unaotishia kutoweka kwa rasilimali hiyo. "Mwaka 1987, marufuku ya uvunaji wa mikoko nchini kote ilitangazwa na Mkurugenzi wa Misitu,"Usimamiaji Shirikishi wa Mikoko. Na mwaka 1991, Mpango wa Taifa wa Kusimamia Mikoko ulianzishwa ambapo rasilimali hiyo iliwekwa chini ya udhibiti wa Mkurugenzi wa Misitu ambaye ndiye pekee mwenye mamlaka ya kutoa kibali kwa mtu yoyote kukata mikoko. 
SOTE KWA PAMOJA TUNAHAKI YA KUSIMAMIA NA KUTUNZA MITI HII YA MIKOKO KWA FAIDA YETU,VIZAZI VIJAVYO NA VIUMBE VINGINE VINAVYOISHI KWENYE MAJI.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

Powered by Teknotaarifa