Saturday, 28 May 2016

JE UNAFAHAMU VIGEZO 9 MUHIMU KABLA HUJAFUGA SAMAKI? AQUES LTD INAKUJIBU.Eneo linalofaakwa ufugaji wa samaki linatakiwa liwe na sifa zifuatazo:

1.       Maji safi, salama na yakutosha kujaza bwawa katika kipindi cha muda mfupi kutoka vyanzo kama chemichemi, visima virefu,mto au mfereji wa kumwagilia;

2.       Eneo lisilo na migogoro ya matumizi ya maji na ardhi;

3.       Udongo ulio na kiasi kikubwa cha mfinyanzi, kwani unauwezo mzuri wa kushika maji. Lakini mfinyanzi ukiwa kwa 100%wakati wa ukame kingo za bwawa zinzwezakupasuka. Hivyo basi  udongo mzuri ni wenye mchanganyiko wa  kiasi kikubwa cha mfinyanzi na aina nyingine za udongo.

4.       Ulinzi ni muhimu kuepuka upotevu wa mali zako

5.       Nguvu kazi, ni muhimu katika eneo lako utakalo anzisha mradi wako wa kibiashara pakawa na uhakika wa kupata wafanyakazi bila kutumia gharama kubwa, kama vile kuwasafirisha na maladhi.

6.       Miundombinu, sehemu utakapoweka mradi wako ni vizuri pawe panafikikika kirahisi.Hii itasaidia gharama za uendeshaji, pia wakati wa mavuno ni rahisi kupeleka bidhaa yako sokoni bila kuharibika.

7.       Mbegu , kabla hujajenga bwawa ni muhimu sana kufanya maandalizi ya mahara pa kupata  mbegu bora  kwa wakati na uhakika

8.       Chakula, pia nimuhimu  kujua samaki wako utawalisha chakula gani.

9.       Soko, kwa sasa samaki bado kuna soko kubwa, cha muhimu nikujua wateja wako wanahitaji samaki aina gani? Na mwenye ukubwa gani?

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa