Saturday, 14 May 2016

JIFUNZE NAMNA YA KUANDAA MNOFU WA KAMBALE.

 Watu wengi wamekuwa wakihofia sana kula kambale kwa vile muonekano wao jinsi ulivyo,lakini leo hii Aques inajaribu kuwafundisha watu namna ya kuuandaa samaki huyo ili mlaji anapo muona asijue kabisa kuwa ni kambale yule ambaye amezoea kumona.
Hatua ya kwanza kabisa baada ya kumvua samaki wako kambale,muoshe kwa maji ya maji ya uvugu vugu ili kuondoa shombo na uterezji alionao ambapo kufanya hivyo utakuwa umepunguza kabisa kiwangio kikubwa cha shombo cha samaki huyo.
Hatua ya pili mtoe mautumbo na vitu vingine vilivyotumboni kwake kwa kumpasua vizuri kabisa.
Hatua ya tatu anza kumkata kata vipande katika saizi unayoipendelea kuitumia au mteja anayopendelea.
Hatua ya nne mchane katikatui ili kuondoa mfupa mkuu wa samaki kasha ondoa upande mmoja kasha fuatia upoande mwingine.
 Hakikisha kuwa vipande hivyo unavyo vikata visiwe na miiba mikuu ya katika au nyama kubwa ikabaki kwenye mfupa,tazama picha hapo inavyoonekana namna ya utoaji wa minofu ya samaki.
 Baada ya hatua hizo zote kukamilika vipange vizuri vyako,kichwa cha kambale unaweza kukiandaa kwa kutengeneza supu yako binafsi na familia.

 Anza kuhifadhi minofu yako vizuri katika mifuko uliyoindaa kwa ajili ya kuhifadhia samaki wako.
 Minofu ikiwa tayari imehifadhiwa vizuri kwa vihifadhio vyake tayarin kupelekwa sokoni au kuliwa kama matumizi ni muda huo huo.Ni vema ukahifadhi samaki kwenye jokofu linalogandisha vizuri na kwa wakati mfupi.
Minofu ya samaki aina ya kambale wakiwa wamehifadhiwa kwenye jokofu tayari kwa matumizi ya siku zijazo.
Leo hii tumewaletea njia hii nzuri na pia ni rahisi kiasi ambacho kitaongeza idadi ya walaji kwa vile muonekano huo ni vigumu mtu kuamini kuwa ni kambale yule ambae alikuwa anamuona hafai mbaya ama hata wengine kumfananisha nyoka,lakini kwa kufanya hivyo utakuwa umeongeza thamani ya samaki wako hivyo ukiwa nao wengi ni rahisi hata kusambaza kwenye migahawa na mahoteli makubwa ambayo hupendelea sana kula minofu.
Njia ni tofauti na ile iliyozoeleka ya ukaushwaji ambayo huchukua muda mwingi kuandaa na pia hupenguza mvuto kwa walaji.
Kama umevutiwa na uandaaji huu kwa maswali au ushauri wasiliana nasi kwa mawasiliano yetu hapo juu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa