Saturday, 28 May 2016

JUA SABABU ZINAZOFANYA WATANZANIA WAFUGE SAMAKI.


Sababu zifuatazo hapa chini zinatoa jibu la kwa nini Mtanzania ufuge samaki;

-Ongezeko kubwa la uhitaji wa samaki ndani na nje ya nchi yetu kunakofanya samaki waliopa sasa kutotosheleza mahitaji.

-Kupungua kwa samaki asili kwenye mito, maziwa na bahari kunakotokana na uvuvi wa kupindukia na haramu.
Kuna upungufu mkubwa sana wa protini duniania na hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania inayotokana kwa asilimia kubwa na vyakula vya aina ya nyama. Upungufu huu wa protini ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya kiafya ya binadamu hasa watoto wadogo na vijana wa umri chini ya miaka 25 ambao wanahitaji kukuwa kwa haraka. Ugonjwa wa Kwashako kwa watoto ndiyo matokeo ya upungufu wa protini mwilini.
 
Urahisi wa kufuga samaki kwa vile hawahitaji eneo kubwa na chakula kisichokuwa na gharama kubwa.
-Wanauwezo wa kutoa mazao mengi (faida kubwa) katika eneo dogo tena ndani ya muda mfupi (uvunaji huanza baada ya miezi mitatu au mine hivi na uvunaji wa mwisho kati ya miezi 6 hadi 12).
Ufugaji wa samaki utasaidia familia kupata kitoweo pasipo gharama za ziada na tena utapata protini ya uhakika.
-Upatikanaji wa maji maeneo mengi ya nchi yetu hasa angalau kwa muda miezi michache kwa mwaka kiasi cha kutoa fursa ya kuzalisha samaki katika kipindi ambacho maji yanakuwepo. Lakini pia maeneo yenye maji ya bomba yanaweza kuzalisha samaki muda wote wowote.
Samaki wanavumilia sana magonjwa, hata mazingira duni wanauwezo wa kuishi
-Ardhi tuliyonayo maeneo mengi ya Tanzania inakidhi ufugaji wa samaki
 
 

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa