Saturday, 28 May 2016

KUSAFISHA NA KUTUNZA MAZINGIRA SIO JUKUMU LA PAUL MAKONDA AU VIONGOZI WA NCHI PEKEE YAO.


Usafi wa mazingira  ni njia ya kuendeleza afya kwa kuzuia mawasiliano ya binadamu na athari za taka. Athari hizo zinaweza kuhusu mwili, mikrobiolojia, biolojia au kemikali vikolezo vya ugonjwa.
Taka ambazo zinaweza kusababisha matatizo ya afya ni kinyesi cha binadamu na wanyama, taka ngumu, maji machafu, taka zaviwandani, na taka za kilimo.
Usafi kama njia ya kuzuia maradhi unaweza kutumika kwa ufumbuzi handisi (kama majitaka na tiba ya maji machafu), teknolojia rahisi kama vyoo, au matendo ya usafi binafsi (kama uoshaji wa mikono kwa sabuni).
Usafi wa mazingira kama unavyoelezwa kwa ujumla na Shirika la Afya Duniani (kwa Kiingereza World Health Organisation, kifupi WHO), unahusu utoaji wa vifaa na huduma ya usalama wa mkojo na kinyesi cha binadamu.
Upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi duniani kote. Uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kwa afya ya wote katika kaya na katika jamii.
Usafi wa mazingira unahusu pia udumishaji wa ratiba ya usafi, kwa njia ya huduma kama vile ukusanyaji wa taka na maji machafu.

Umuhimu wa kutenga taka upo katika jitihada za kuzuia maji na usafi wa mazingira kuhusiana na ugonjwa, ambayo inaadhiri nchi zilizoendelea na zinazoendelea kwa viwango mbalimbali. Inakadiriwa kuwa hadi watu milioni 5 wanakufa kila mwaka kutokana na magonjwa yanayozuilika yanayotokana na maji [5] , kwa sababu ya upungufu wa usafi na usafi wa mazingira. Athari za usafi wa mazingira zimeathiri jamii pakubwa. Katika kitabu cha Griffins usafi wa mazingira ya Umma utafiti wa Usafi wa Mazingira unaonyesha kuwa hali ya juu ya usafi wa mazingira inaleta mvutio maishani.
 
Mazingira yaliyozungukwa na viwanda yanatishia amani kwa jamii yetu ya Tanzania hasa kwa watu wanaoishi  katika maeneo  haya yanayozungukwa na viwanda.
Watu waishio katika mazingira haya wanapata taabu sana kutokana na moshi unaotoka katika baadhi ya viwanda na mazingira machafu yaliyopo nje ya viwanda hivyo.Baadhi ya watu waishio katika mazingira  haya  wanailalamikia  serikali kwani imewasahau sana wanapopeleka malalamiko yao serikalini hayashughulikiwi ipasavyo.Hivyo wanaiomba Serikali ijaribu kuwafuatilia watu hawa wanaomiliki viwanda hivi ili waweze kujali afya za watu wanaoishi katika mazingira haya.
Utumiaji wa mazingira ni wetu sote na utunzaji wa mazingiza unatugusa wote hivyo  kila mmoja anapaswa kuweka mazingira katika hali ya usafi na utumiaji bora kwa afya .

 AQUES LTD NI MOJA YA KAMPUNI INAYOJIHUSISHA PIA NA MASUALA YA MAZINGIRA KUHAMASISHA JAMII KUFAHAMU MAANA YA MAZINGIRA NA UMUHIMU WAKE HIVYO SIO SUALA LA KUMTEGEME KIONGOZI FULANI AFANYE AU KIKUNDI FULANI ILA NI JUKUMU LA KILA MTU ANAPASWA KUTUNZA NA KUSAFISHA MAZINGIRA KILA SIKU NA SIO KWA SIKU MAALUM.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa