Saturday, 28 May 2016

Serikali ziwekeze katika ufugaji wa samaki ili kuinua sekta hiyo: FAO

Ripoti mpya ya Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO imesema sekta ya ufugaji wa samaki katika maji baridi na baharini barani Afrika inaweza kuwa na mchango mkubwa zaidi kwa uchumi iwapo serikali zitawekeza zaidi tofauti na sasa ambapo ufugaji huo ni wa kiwango kidogo na unatia hofu kwa walaji.
Alessandro Lovateli kutoka Idara ya samaki na ufugaji samaki ya FAO ameiambia idhaa hii kwa sasa sekta hiyo inakua lakini mchango wake katika soko la kimataifa inaweza kuwa kubwa zaidi iwapo…
 “Kile tunachotaka kushuhudia pale ni kuanzishwa kwa teknlojia sahihi, na kuhakikisha kuwa ufugaji samaki unachukuliwa kama biashara. Tunahitaji kusaidia nchi kuanzisha miradi ya biashara badala ya miradi midogo ya vijijini. Hiyo miradi midogo inaweza kujumuishwa! Nchi zinapaswa kutambua kuwa kuna fursa ya kuanzisha ajira, chakula zaidi kwa wananchi na pia kwa kuuza nje ya nchi."
Ametaja Ugandakuwa mfano wa mafanikio ya ufugaji wa samaki aina ya Sato katika maji baridi ilhali Msumbiji iko mstari wa mbele katika ufugaji wa samaki aina ya Kamba baharini.
Amesema kuna hofu ya uharibifu wa mazingira katika ufugaji wa samaki aina ya kamba baharini hususan ukataji wa mikoko, lakini FAO kwa kushirikiana na mashirika mengine fufanya kazi kubwa ya kusaidia jamii kufahamu fulsa zilizopo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa