Saturday, 14 May 2016

WAFUGAJI TUWE NA TABIA YA KUPIMA UZITO SAMAKI WETU KUJUA MAENDELEO YA UKUAJI WAO NI MUHIMU SANA.

Habari ndugu wasomaji wetu,Aques Ltd kama ilivyo kawaida yake haitosita kutoa elimu juu ya ufugaji wa samaki nchini na kuwakumbusha juu ya yale yanayopaswa kufuatwa ili ufugaji wa samaki uwe na tija kwa wafugaji wa samaki hapa nchini.
Kuna umuhimu mkubwa sana kupima samaki uzito kila baada ya muda kadhaa eidhaa kila baada ya mwezi mmoja angalau ili kujua samaki wako wanaendeleaje haswa kujua uzito wao.Kujua uzito au ukuaji wa samaki utakusaidia kujua sasa kwa muda huo samaki wako wanakula kiasi gani ilio samaki wako akuwe vizuri,hatua hii ni muhimu sana kuifanya nasio  kulisha samaki kwa mazoea au makadilio tu kwenye makopo au viganja vyetu.
Aques ltd inawasisitiza sana katika utekelezaji wa suala hili kwani ni muda ya kitu muhimu sana kinapaswa kifanyike kwenye mradi wako,unaweza kuwa na mzani wa digitali kama unavyouona kwenye hiyo picha ambao hupatikana kwa bei ndogo sana kati ya 20,000-30,000 kitu ambacho kila mfugaji anaweza kuwa nao na pia kutumia mzani huo kupiuma chakula chake ili kulishia samaki kwa uzito stahiki na kwa wakati husika.

 Wafugaji wakitoa samaki kwenye bwawa kuangalia maendeleo yao.
 Mfugaji akiweka sawa kumbukumbu ya matokeo baada ya kupima uzito wao.

Samaki ambao wamechuliwa sampuli aina ya kambale na sato.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa