Saturday, 28 May 2016

WAHITIMU WA VYUO HUWA MNAJIWEKEA MALENGO GANI KABLA YA KUINGIA MTAANI?.

Nchi yetu ni mmoja ya nchi yenye fulsa kubwa sana kiuchumi,ukiamua kufanya chochote kile ilimradi kiwe kimefuata sheria za nchi bila kuathiri chechote kile basi biashara hiyo itakulipa sana.Tumeshuhudia vijana wengi sana wakifanikiwa kimaisha kupitia kilimo na ufugaji,lakini wengi wao huchukua hatua hizo baada ya kushindwa kuendelea na ngazi nyingine ya elimu,lakini maskini ya mungu pasi kujua kile anachoenda kukifanya ndio kina mtoa kimaisha.
Vijana wengi huingia chuo wakiwa na ndoto mbalimbali lakini wachache wao husikia nataka kujiari mwenyewe,kijana huyo anayetamka hiyo kauli huchekwa sana na wenzake kwani wengi wao hufikilia zaidi kuajiriwa kukaa kwenye ofisi kubwa yenye kiyoyozi na kila aina ya vito vya samani.
Hapa na kutana na mtaalamu aliyebobea katika masuala ya sayansi ya viumbe maji bwana JAMES ALFREDY kutoka chuo kikuu Dar es salaam ni wanafunzi wachache sana ambao husoma wakiwa na ndoto za kutaka kuwa na nani na dhamira ya kutoa mawazo yake kwa wengine bila gharama yeyote na kufanikiwa,bwana James anasema vijana wengi ni waoga wa kuthubutu kufanya jambo fulani wakihofia kushindwa wakati hawajajaribu hilo wazo alilokuwa nalo.
Vijana wengi wanapokosa ajira hupendelea kuendelea na ngazi nyingine ili kupata ajira kirahisi bila kuifanyia kazi ile aliyoipata kwanza.
Hapa bwana james anatoa fasili ya neno "elimu ni ile inayo weza kumsaidia mtu ili kukabiliana na changamoto  zinazomakabili yeye au jamii yake inayomzuunguka ili kujenga taifa imara na salama zaidi" hivyo kama kijana umesoma alafu hujafanikiwa kutatua changamoto yeyote katika taifa lako hapo ni sawa hujapata elimu au umeshindwa kuitumia elimu yako,unaweza ukawa umeshia darasa la saba,kidato cha nne au cha sita na ukafanikiwa kuisaidia jamii kukabilina na changamoto fulani katika jamii eidha katika kilimo,uvuvi ufugaji,au watu walikuwa hawaelewi vizuri kuhusu demokrasia ukafanikiwa kuwaelewesha na wakaelewa hapo utakuwa umeitumia vizuri elimu lakini pia utakuwa ni sehemu yako ya ajira kupitia hicho ulichotoa kwa jamii yako.

Bwana James Alfredy anaeleza kuwa ni vyema sasa vijana kujifunza mfumo wa kujiari kwani mataifa yaliyoendelea yamepiga hatua kubwa kwa wanavyuo kujiari wenyewe,na hapa sio lazima uwe na mtaji mkubwa cha kwanza kabisa ambao ndio mtaji wako ni fikra,unafikilia kufanya nini kwanza?Akatolea mfano kidogo wakati anachukua shahada ya pili (masters) alikuwa na rafiki yake kutoka chuo cha uvuvi mbegani aliyehitimu stashada ya ukuzaji viumbe maji (AQUACULTURE) yeye fikra yake alikuwa na wazo la kufungua blog ilikuelimisha jamii juu ya miradi ya ufugaji wa samaki baada ya kuona changamoto yeye wakati anasoma alikuwa hapati taarifa za masuala ya ufugaji au habari ufugaji samaki hapa nchini,hivyo akaona vyema kufungua blog ili kuisaidia jamii yake na wanafunzi wa kada yake waweze kuapata taarifa kirahisi.Bwana James anaeleza kuwa rafiki yake kwanza kabisa alikuwa na wazo ambacho ni kitu muhimu sana ili unapoenda kuomba ushauri iwe nyiongeza wa kukuza na boresha wazo lako liweze kufanikiwa,ni kweli rafiki yangu nilimsaidia kuendeleza wazo lake hilo na hatatimaye kufanikiwa kufungua blog yake hiyo bureee bila gharama yeyote ile kupitia GOOGLE,lakini sasa ivi kijana huyo anatoa ajira kwa wengine amenunua mashamba na viwanja  na pia kuanzisha mradi wake mwenye wa ufugaji wa samaki.
Kitu kikubwa ambacho wahitimu utasikia wakisema mitaji bila kufikilia kwanza bishara aitakayo na pia wahitimu walio wengi hupenda kuwa na wazo la kutaka mitaji mikubwa jambo,sio rahisi kufanikiwa katika mifumo ya kimaisha.
Hivyo vijana wengi sasa wanaotoka vyuoni kujifunza zaidi namna ya kujiari wenyewe wanapotoka masomo ili waache kutegemea serikali ambayo tayari imeshaweka fulsa za kutosha kutumia rasilimali zao bila kusubili wageni kuja kuzitumia.Akitolea mfano wanaweza kuanzisha miradi yakufuga samaki na kufanikiwa kimaisha pia kujiunga katika vikundi kusaidia kupata mikopo kirahisi kutoka taasisi za kifedha.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa