Wednesday, 22 June 2016

EWE MVUVI ACHA UVUVI HARAMU!NI HATARI!

Uvuvi ni kazi ya kukamata samaki na pia ufugaji wa samaki na wanyama wengine wa maji. Kusudi lake ni hasa kupata chakula lakini siku hizi uvuvi unatokea pia kama burudani, katika utalii na kama sehemu ya michezo.
Uvuvi ni kati ya shughuli za kale kabisa za binadamu na katika uchumi huhesabiwa katika sekta ya msingi pamoja na kilimo na uchimbaji wa madini. Kutokana na takwimu za FAO kuna watu milioni 38 dunani wanaofanya kazi ya kuvua au kufuga samaki. Pamoja na wengine wanaosafirisha windo na kulifanyia kazi viwandani au kuiuza masokoni, madukani au kwenye hoteli kuna zaidi ya watu milioni 500 wanaopata maisha yao na sekta hii ya uvuvi.

uvuvi ni mojawapo ya shuguli za binadamu ambayo ina shughulika na ukamataji wasamaki kutoka ndani ya maji na kuwekwa nje ya maji. pia samaki hao hufanywa kama kitoweo na muda mwingine hufanywa kama biashara ili kujipatia kipato na pia uvuvi nao husaidia kukuza uchumi wa nchi fulani.
Uvuvi hufanywa penye magimba ya maji kama kwenye bahari, maziwa, mito au mabwawa. Mara nyingi wavuwi hutumia chombo cha maji kama boti lakini wengine wanakaa ufukoni na kuvua kutoka nchi kavu.

Vyombo vya uvuvi ni aina za nyavu zinazoweza kushika samaki yote na kuivuta nje ya maji, ndoano au pia aina za mikuki inayolenga samaki zilizipo karibu na uso wa maji.
Tunapaswa kulinda bahari,maziwa pamoja na mito ili mazalia ya samaki yazidi kuongezeka na pia tupige vita uvuvi haramu kuwa husababisha kuwa nyuma kwa sekta ya uvuvi ==Nashauri serikari iweke ulinzi kwenye swala la uvuvi kwani kuna wavuvi haramu wanaotumia sumu,baruti na vingine vingi ambavyo havitakiwi katika uvuvi.


0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa