Tuesday, 19 July 2016

FAHAMU ALICHO ONGEA WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI MH.DR CHARLES J.TIZEBA.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Dr. Charles John Tizeba amewataka wafanyakazi wa wizara yake kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mhe. Dr. Tizeba alitoa wito huo wakati akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa wizara hiyo katika siku yake ya kwanza alipofika wizarani kuanza kazi rasmi.
“Kufanya kazi kwa pamoja tutaweza kufikia malengo yaliyokusudiwa , kitendo cha kutoshirikiana ndani ya wizara haitatufikisha po pote’’ alisitiza Mhe. Dr. Tizeba.
Mhe. Dr. Tizeba pia aliwataka watumishi wote ndani ya wizara kufanya kazi kwa kutoa ufumbuzi na majibu ya changamoto mbali mbali pasipo kumtegemea yeye kwa kuwa hana majibu kwani wao ndio watalaamu.
Aliwatahadharisha kutopeleka madokezo yenye kutafuta ufumbuzi kwake vinginevyo atachukua hatua kali.
‘’ Nawaomba mniandikie ushauri na si kuniandikia kutaka majibu toka kwangu, nyie ndo watalamu” aliongeza Mhe. Dr. Tizeba.
Tuwe watu wa kutoa majibu katika changamoto zetu na si kuningoja mimi nitoe majibu mie si mtalaamu.
Kitu kingine alichoongelea Dr. Tizeba ni kufanya kazi pasipokuwa na nidhamu ya uoga. 
Aliongeza kuwa watu wenye nidhamu ya uoga huwa wanatoa ushauri ambao si sahihi kutokana na kuwa wamejaa hofu katika utendaji wao wa kazi.
‘’ Nisingependa kuwa na watu wenye tabia ya uoga tuwe huru na kupeana heshima inayostahili kuliko kuwa na nidhamu ya uoga’’ alifafanua Mhe. Dr. Tizeba.
Mhe. Rais Dr. John Pombe Magufuli alimteua Mhe. Dr. Charles John Tizeba, Mbunge wa Buchosa kuwa Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi kuchukua nafasi ya Mhe. Mwigulu Lameck Nchema aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa