Thursday, 21 July 2016

HII NDIO NJIA PEKEE YA KUZUIA NDEGE KWENYE BWAWA LA SAMAKI.

Kumekuwa na changamoto nyingi sana kwa wafugaji wa samaki lakini changamoto kubwa ambayo hulalamika ni juu ya ndege.Ndege hula samaki wanapoingia ndani ya bwawa la mara nyingi hula kwa kuvizia pindi usimamizi unapo kuwa umelega lega hivyo ndige huchukua samaki aliye ndani ya bwawa la samaki.
Madhara makubwa ya ndege kuchukua samaki hiyo ni kupelekea kupungua kwa idadi ya samaki kwenye mabwawa hali inayo pelekea upungufu wa samaki siku ambayo mfugaji anapofanya mavuno.
Utakuta mfugaji analalamika sana kuwa nimeweka samaki 3000 au 4000 lakini siku mwisho ya mavuno huambulia samaki 1500,2000 au Zaidi ya hapo lakini sio sawa na idadi ile aliyopandikizwa kwenye hivyo hupelekea hasara  kwa mfugaji.
AQUES LTD na timu yake ya wataalamu hufanya kazi ya kudhibiti ndege hao na wadudu wengine wanaoingia kwenye mabwawa na kushambulia samaki.Fuatilia hatua hizo hapo chini namna ya kuweka nyavu ili kudhibiti tatizo hilo.
 Picha ikionesha ndege akichukua samaki kutoka ndani ya bwawa.

 Nyavu maalum ambayo huwa na matundu madogo huzui ndege kutua kabisa ndani ya bwawa na sio ndege tu pekee yao bali hata wadudu huzuia kuingia ndani ya bwawa lako na kufanya ulinzi ulio imara na kupunguza malalamiko ya upotevu wa samaki ndani ya bwawa lako.

Picha ikionesha moja ya mabwawa yaliyo jengewa wavu maalum kwa ajili ya kudhibiti ndege na wadudu wengine hatarishi kwenye mradi wa ufugaji wa samaki.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa