Saturday, 23 July 2016

HII NDIO NJIA SAHIHI YA UCHIMBAJI WA MABWAWA YA KUFUGIA SAMAKI.

Njia sahihi kabla ya kuanza mradi wako ili uende vizuri na uwe na tija kubwa katika biashara yako ,kumekuwa na tabia ya watu wengi kuanza miradi hii pasi na kupata ushauri kutoka kwa wataalam ni namna gani mradi huu unapaswa uanze ili kupunguza gharama za uendeshaji wa mradi wako.
Wataalam kazi kubwa ni kukushauri vema namna ya kuanza mradi wako.Kabla ya kuanza mradi wataalam wanapaswa kuona eneo lako na kukugua na kuchunguza kwa kina ni vitu gani vitahitajika ili uchimbaji wa mabwawa uanze.
Uchimbaji huu unaweza kufanyika kwa njia ya mitambo kama kampuni ya AQUES LTD inafanya ni kutumia mashine maalum za uchimbaji wa mabwawa kwa gharama nafuu hivyo kufanya mabwawa yako yakamilike kwa muda mfupi tofauti kabisa na uchimbaji wa mikono.

Utumiaji wa uchimbaji wa  mabwawa kwa kutumia mikono yaani sepetu ,sululu n.k unaweza kufanywa pale tu mradi unapokuwa mdogo na ardhi isiyokuwa ngumu.Lakini endapo mradi ni mkubwa baada tathimini ya wataalam baada ya kuona eneo lako ndipo utashauriwa kutumia njia ipi sahihi kwa ajili ya kuanza mradi vema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa