Friday, 22 July 2016

JUHUDI PEKEE NDIO NJIA YA KUJIKOMBOA NA UMASKINI.

Juhudi pekee ndio njia ya kujikomboa na umaskini ni kauli yake kijana Ibrahimu Danda ambaye pia ni mtaalamu wa uchakataji na uhifadhi samaki katika ubora kutoka chuo cha maendeleo ya uvuvi mbegani Bagamoyo kwa sasa kinatambulika kama Wakala wa elimu na mafunzo ya uvuvi (FETA).Anasema Juhudi pekee ndio njia ya mafanikio katika kufikia malengo yake,hakika kila binadamu anatamani sana kuwa tajiri lakini bila juhudi,mafanikio au utajiri utabaki kusikia kwa wengine.
 Ibrahimu Danda amekuwa kijana wa mfano sana katika juhudi zake kupitia taaluma yake akihamasisha kwa vitendo na wavuvi wadogo wadogo ili kuwaongezea uelewa ili kutambua na kuelewa ni namna gani wanaweza kufikia malengo yao katika shughuli zao za uvuvi na kuhamasisha kuachana na uvuvi wa mazoea ambao muda mwingi umekuwa hauna tija kwao,licha ni hivyo amekuwa akiwaeleza athari za uvuvi haramu kwa upande wao na taifa kwa ujumla.
Katika kuhakikisha wavuvi wanabadilika kifikra ana waeleza juu ya fulsa ya ufugaji wa samaki ambayo ni njia mbadala kwao badala ya kufanya uvuvi jambo wamekuwa wakishindwa kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.Wavuvi wengi wanapaswa kujikita zaidi katika ufugaji wa samaki ili kuongeza kipato chao pia wanaepuka hadhaa ambazo wanakutana nazo wanapokuwa wanavua.
Endepo vijana wengi wanapohitimu wakazitumia hizo taaluma zao kwa watapata mafanikiomakubwa hivyo yeye atakuwa chachu kwa maendeleo yake binafsi na taifa kwa ujumla.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa